Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary
Masanja (Mb) akizungumza na wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania,
Wilaya ya Misungwi, alipotembelea ofisi
hiyo leo kwa ajili ya kuzungumza namna bora ya kuinua mapato ya jumuiya hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa mizinga ya nyuki 50 ili kuunga mkono mradi wa ufugaji nyuki wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Misungwi.
Ameyasema hayo leo alipotembelea Ofisi za
UWT Wilaya ya Misungwi ikiwa
nimwendelezo wa ziara zake katika mkoa wa Mwanza za kuangalia namna ya
kuanzisha miradi katika ofisi za UWT za mkoa huo.
“Kati ya mambo ambayo natamani mfanye ni kuwa
na miradi ya kujitegemea na hapa nimesikia mna mizinga ya nyuki mitano, Mwenyekiti
ninaahidi nitaongeza mizinga hamsini ambayo itakuwa ni mradi wa UWT hapa
Misungwi” Mhe. Masanja amesema.
Pia, Mhe. Mary Masanja amekabidhi fedha za
kuwekeza kwenye miradi yenye thamani ya shilingi 14, 650,000 kwa mchanganuo
ufuatao;mitaji ya biashara shilingi 7,700,000, mitungi ya gesi 70 yenye thamani
ya shilingi 2,800,000, pikipiki moja yenye thamani ya shilingi 2,550,000 na kompyuta
moja yenye thamani ya shilingi 1,600,000 kwa kinamama wa Jumuiya ya Umoja wa
Wanawake Tanzania, Wilaya ya lengo ikiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Naye, Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Misungwi,
Mhe. Angela Gabriel amempongeza Mhe. Mary Masanja kwa kuisaidia jumuiya hiyo.
“Tuna furaha isiyopimika na tumpongeze Mhe.
Mary Masanja kwa kuwa mambo anayoyafanya ya kutukabidhi mitaji na majiko ya
gesi hayajawahi kutokea katika Wilaya yetu ya Misungwi, tunakushikuru sana”
amesisitiza. Mhe. Angela.
Mhe. Mary Masanja yupo Mkoani Mwanza kwa ajili
ya ziara ya kutembelea ofisi za UWT mkoani humo kwa lengo la kuangalia namna
bora ya kuanzisha miradi itakayoongeza mapato ya jumuiya hizo.
No comments:
Post a Comment