Habari za Punde

Wizara ya Elimu ya Mafunzo ya Amali Imefanya Mabadiliko katika Ngazi ya Elimu ya Msingi Kurejesha Darasa la Saba Mwakani 2022.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar kuhusiana na kurejeshwa kwa Darasa la Saba Zanzibar, mazungumzo hayo yamefanyika ukumbi wa Wizara ya Elimu mazizini Jijini Zanzibar.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha TV cha Island Rashid akiuliza swali wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kutoa taarifa ya kuaza kwa Darasa la Saba.


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imefanya mabadiliko katika ngazi ya elimu ya msingi kwa kurejesha darasa la saba kuanzia mwaka 2022 kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Simai Mohammed Said amesema mabadiliko hayo ni kwa ajili ya kuimarisha  elimu ya msingi kuwa ya miaka saba badala ya sita kama ilivyo sasa.

Waziri Simai amesema kufuatia tathmini zilizofanywa na Wizara pamoja na ushauri wa wadau na wazazi wa Wanafunzi kupitia mijadala mbali mbali wameona kuna haja ya kulifanyia kazi suala hilo kwani Wanafunzi wanaanza elimu ya Sekondari wakiwa na umri mdogo hali inayopelekea matokeo mabaya katika mitihani ya Kitaifa. 

Akizungumzia kuhusiana na mabadiliko ya mitaala amesema Wizara ipo katika hatua za kukamilisha mtaala huo kwa ngazi ya maandalizi na msingi ambapo umezingatia mabadiliko mbali mbali ikiwemo kupunguza idadi ya masomo ambavyo yameonekana ni mengi ukilinganisha na uwezo wa watoto katika kujifunza.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar bw Ali Khamis Juma amesema Wizara itatoa muongozo kwa Baraza la Mitihani kupinga matokeo ya Wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la sita kwa mwaka huu ambapo kwa waliofikiwa ufauli wa asilimia 60 ndio  watakaoendelea na masomo ya kidato cha kwanza na waliopata asilimia 40 ndio watakaondelea na masomo ya darasa la saba.

Nao baadhi ya Wanafunzi wamepongeza hatua hiyo ya Serikali kwani imeonekana Wanafunzi na wazazi walio wengi walikuwa wakitoa malalamiko yao juu ya watoto wao kupeleka Sekondari wakiwa na umri mdogo ambao bado hawajatambua thamani ya elimu yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.