Habari za Punde

Habari za Hivi Punde: Ajali kubwa ya Boti Kisiwa Panza

 Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raajiu'un

Kumetokea msiba mkubwa kisiwa Panza Pemba ambapo watu 11 wamefariki na wengine 15 kuokolewa katika ajali ya boti waliokuwa wakitoka nayo msibani kisiwa Panza kuzamamajira ya saa 12.30 za magharibi.

Maiti 11 zilizopatikana zimehafidhiwa katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba ambapo ndugu na jamaa wanakwenda kuzitambua.

Waokoaji kutoka kikosi cha KMKM bado wapo wakiendelea kutafuta watu wengine.

Pia kwa mujibu wa taarifa kuna watu wengine 14 bado hawajulikani walipo kwani boti inakisiwa kubeba kama watu 40 waliokuwa wakitoka Chokocho kuelekea kisiwa Panza mazikoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.