Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Philip Mpango akiagana na
viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar
es salaam wakati akiondoka nchini kuelekea Lilongwe nchini Malawi kumuwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano
wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 12 Januari 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Philip Mpango hii leo
tarehe 10 Januari 2022 anaondoka nchini kuelekea Lilongwe nchini Malawi
kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wananchama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 12 Januari 2022.
Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa , Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) utakaofanyika tarehe 11 Januari 2022.
Franco Singaile
MMR – Habari. Januari 10,2022.
No comments:
Post a Comment