Habari za Punde

Mhe Hemed mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa mashine kumi za kusukumia maji

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Salha Mohamed Kassim akimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais kuwa mashine zilizotolewa na mfabiashara Hassan Raza zitatumiwa kama zilivyokusudiwa katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama.
Mhe. Hemed akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya mashine kumi za maji iliofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakili ambapo amemshkuru mfanyabiashara Hassan Raza kwa moyo wake wa kizalendo katika kuinga mkono serikali
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipokea Mashine kumi za Maji (Water Pump) zilizotolewa na mfanyabiashara Hassan Raza ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyoiweka.


Na Abdulrahim Khamis, OMPR

Jumla ya Mashine kumi(10)  za kuskumia maji (Water Pump) zenye Gharama ya Shillingi Millioni Mia moja na hamisini zimetolewa na Mfanyabiashara Hassan Raza na kukabidhiwa kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar zinazolenga kwenda kutatua tatizo la upatikanaji wa wa Huduma ya maji safi na salama.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alimpongeza na kumshukuru mfanyabiashara Hassan Raza kwa kutekeleza ahadi yake  kupitia hafla fupi ya kukabidhi pampu hizo iliyofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Alisema serikali inathamini mchango unaotolewa na Wafanyabiashara nchini ambapo Zoezi la kukabidhi Pampu hizo litaweza kutoa nafasi kwa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kuweza kuendesha shughuli zao za kila siku za kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mhe. Hemed aliutaka uongozi wa Mamlaka wa maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha Pampu hizo zinatumika katika maeneo husika kama ilivyoahidiwa, ili kuhakikisha huduma hiyo inawafikia walengwa.

Nae Waziri wa Maji, nishati na Madini Mhe. Suleiman Masoud Makame alimshukuru mfanyabiashara huyo kwa kitendo chake hicho, na kuwataka wafanyabiashara wengine kuiga mfano huo wa kuisaidia serikali kwq pamoja katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Salha Mohamed Kassim alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZAWA inachukua jitihada mbali mbali za kupunguza tatizo la maji ambapo kukabidhiwa kwa Pampu hizo inakwenda sambamba na malengo ya maendeleo endelevu ya Dira ya maendeleo ya Mwaka 2025 na mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUZA III).

Aidha Dk. Salha alimshukuru mfanyabiashara huyo kwa kuendelea kuiunga mkono serikali katika kufikisha huduma mbali mbali za kijamii akieleza kuwa utoaji wa Pampu hizo ni Dhahiri kuguswa kwake kwa tatizo la ukosefu wa maji mijini ja vijijini

Kwa upande wake Mfanyabiashara Hassan Raza alisema zoezi la utoaji wa Pampu hizo ni kutekeleza Ahadi aliyoitoa kwenye kikao cha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibari pamoja na wafanyabiashara ambapo aliwata kwa umoja wao kuunga mkono serikali katika kutatua tatizo la maji nchini.

Mapema  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alijumuika na waumini wa Masjid Weles Kikwajuni katika Ibada ya sala ya Ijumaa ambapo amewataka wazanzibari kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo nchini.

Mhe. Hemed alieleza kuwa serikali imetenga fedha kwa ajili ya uwezeshaji ambapo serikali itabeba gharama zote za Miundombinu katika maeneo yaliopangwa ili kurahisisha usalama wao na Mali zao.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.