RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika maziko ya Marehemu Safia Abeid Mama Mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt. Mohammed Bilal,Mtoto wa Marehemu Bw. Abeid, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf Alhaj Balozi Seif Ali Iddi,yaliyofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj.Dkt.Mohammed Gharib Bilal akiweka mchanga katika kaburi la Mama Yake Mzazi Marehemu Bi.Safia Abeid,baada ya kuweka mwili wa marehemu maziko yaliyofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 4-1-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Bi.Safia Abeid, Mama mzazi wa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, maziko yaliofanyika Kijiji kwao Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Alhaj Dkt.Mohammed Gharib Bilal, kwa kufiwa na Mama yake mzazi marehemu Safia Abeid, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
04.01.2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj
Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameshiriki mazishi ya Marehemu Bi Safia Abeid, mama
mzazi wa Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed
Gharib Bilal yaliyofanyika huko kijijini kwao Kiboje Mwembeshauri, Wilaya ya
Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa, dini na Serikali, wananchi pamoja na wanafamilia walihudhuria katika mazishi hayo ambapo mapema Alhaj Dk. Mwinyi aliungana nao katika sala ya kumuombea Marehemu iliyosaliwa huko Masjid Jaami Zinjbaar, Mazizini, Jijini Zanzibar.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari.
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment