Habari za Punde

Yanga waishangilie Azam leo



 

Adeladius Makwega

Zanzibar

Mamia ya mashabiki wa timu ya soka ya Simba ya Tanzania wameshuhudiwa leo hii wakielekea Zanzibar ambapo timu yao inatajiwa kucheza na timu ya mpira wa miguu ya Azam zote za Dar es Salaam katika fainali ya Kombe la Muungano, kuhitimisha fainali hizo za mwaka huu.

 Mashabiki hao wakiwa wamevalia jezi na sare zenye rangi nyekundu na nyeupe wakibeba vifaa kadhaa vya kushangilia wakiwa na bashasha kuelekea fainali hiyo.

“Simba hatuna maneno, timu yetu itashinda magoli kadhaa na tuna hakika kombe ni letu.” Alisema Mhusini Abdu-Rahaman ambaye ametokea Mbezi Louise Dar es Salaam, aliyatamka hayo kwa kujigamba huku akishuka boti katika Mji wa Zanzibar.

“Mimi ni mwanachama wa Simba na kila pahala Smba inapocheza nakuwepo ndiyo maana nimelipa 25,000/-kuja Zanzibar kushangilia ushindi na si vinginevyo.”

Alisema Grace Mkocheka akiwa Kariakoo Zanzibar ambaye anatokea Tandika Davies Kona.

Mashabiki hao walionekana wakiwa wamejitwika mabango, vikapu na zana kadhaa za ushangiliaji huku zana hizo zikipambwa na ujumbe wa kuwananga timu ya Azam na hata watani wao wa jadi Yanga.

“Yanga njoni muishangilie Azam”

“Simba chama kubwa.”

“Kapu la magoli VIP B.”

Chakustajabisha mwandishi wa habari hii hakujaliwa kuwaona mashabiki wa Azam katika safari hiyo. Mechi hiyo inahitimisha mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi yanayofanyika kila mwaka kwa kumbukumbu ya mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika Januari 12, 1964.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.