Habari za Punde

*JESHI LA POLISI, KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI ZANZIBAR*,

Jeshi la Polisi Usalama barabarani linawakumbusha na kuwataka madereva wote wa vyombo vya moto wanapoendesha vyombo hivyo kuzingatia na kufuata kikamilifu sheria, kanuni na taratibu za Usalama Barabarani ili kuepuka kusababisha ajali ambazo zinapelekea madhara kwa watumiaji wengine wa barabara  wakiwemo na wao madereva wa vyombo husika,kama vile vifo na majeruhi  mali na uharibifu wa miundo mbinu ya barabara n.k. 

Vyanzo vikuu vya ajali za barabarani  ni pamoja na;

1.*Makosa ya kibinaadam* (uzembe, ulevi, mwendo kasi, kutovaa kofia ngumu/helment, kuzidisha abiria/mshikaki, n.k)

2.*Ubovu wa vyombo vya moto*(magari,pikipiki,n.k)

3.*Mazingira*(Ubovu/ufinyu wa  barabara,Ukungu wakati wa baridi kali/mvua, vumbi, n.k).
Kwa upande wa Makosa ya kibinaadamu  ndio chanzo kikuubwa kinachoongoza kwa kusababisha ajali za barabarani takriban kwa 78%.

Kumekuwepo na matukio ya ajali za barabarani za mara kwa mara zinazosababisha vifo na majeruhi.

-Kundi linaloongoza kwa matukio hayo ya ajali ni waendesha vyombo vya maringi mawili (pikipiki@ bodaboda). Ktk kundi hili wahanga wanaopoteza maisha au kupata madhara makubwa mara nyingi  unakuta mhanga  hakuvaa kofia ngumu.

Kwa mujibu wa sheria, ni kosa kwa mtumiaji wa chombo cha maringi mawili/pikipiki kutovaa kofia pindi anapotumia usafiri huo.Siyo jambo la hiari bali ni jambo la lazima kuvaa kofia ngumu.

Jeshi la Polisi Zanzibar-Kupitia Kikosi Cha Usalama Barabarani  limekuwa likitoa elimu ya usalama barabarani kwa njia ya mbalimbali, ikiwemo, redio, tv, mashuleni, kwenye vijiwe vya bodaboda, vituo vya mabasi, ktk mikutano ya Polisi Jamii,matangazo kwa kutumia magari kwa kupita maeneo mbalimbali  n.k kwa kuwaelimisha juu ya  UTII WA SHERIA BILA SHURUTI.

Pamoja na mikakati hiyo lakini bado baadhi ya madereva siyo wasikivu na matokeo yake watumiaji wa barabara wanaendelea kupata madhara yanayotokana na ajali za barabarani.

HIVYO, Jeshi la Polisi, Kikosi Cha Usalama Barabarani Zanzibar, linawakumbusha na kuwataka madereva wote wa vyombo vya moto kutii na kufuata sheria za barabarani bila shuruti.

Kuacha uegeshagi magari ovyo brbrn(wrong parking),mwendo kasi, kutovaa kofia ngumu, kuzidisha abiria/mshikaki, n.k.*OPERESHENI NA MSAKO MKALI*  itafanyika ktk maeneo mbalimbali kwa kuwakamata wale wote watakaobainika kufanya makosa *HATARISHI* ya Usalama Barabarani  na kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo  kuwafikisha mahakamani.Hakutakuwa na *Muhali* kwa madereva wazembe.

Ili kuepuka usumbufu huo wa kisheria ni vizuri suala zima la UTII WA SHERIA BILA SHURUTI ukazingatiwa na kila dereva na watumiaji wengine wa barabara.

Zanzibar bila Ajali  inawezekana kama kila mmoja *ATATIMIZA WAJIBU WAKE*
USALAMA  BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.

Jeshi la Polisi-Kikosi Cha Usalama Barabarani ZANZIBAR.
17/02/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.