Na Mwashungi Tahir Maelezo
Jumla ya matukio 65 ya ukatili na udhalilishaji wa jinsia yameripotiwa mwezi wa January ,2022 ambapo wengi wao walikuwa ni watoto ambao ni asilimia 75.4 na wanawake ni asilimia 24.8.
Akiwasilisha Takwimu za ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa mwezi wa January 2022 Mtakwimu kutoka kitengo cha makosa ya jinai na jinsia katika ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Asha Mussa Mahfoudh wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu uliopo Mazizini .
Amesema mlinganisho kwa idadi ya matukio kwa mwezi wa Januari imepungua kwa asilimia 13.0 kutoka matukio 97 kwa mwezi wa Disemba 2021 hadi 65 mwezi wa Januaty 2022.
Akitoa taarifa za Wilaya amesema Wilaya ya Magharibi “B” imeripotiwa kuwa na matukio mengi ukilinganisha na Wilaya nyengine matukio 13 zikifuatiwa na Wilaya ya Wete matukio 11 , na Wilaya ya Magharibi “A” matukio 10.;
Kwa Wilaya ya Kaskazini “B” muwasilishaji Asha amesema imeripotiwa kuwa na idadi ndogo ya matukio kuliko wilaya zote tukio moja 1 na wilaya ya Mkoani hakuna tukio lililoripotiwa.
Amesema matukio 54 kati ya matukio 65 yaliyoripotiwa yapo chini ya upelelezi wa Polisi, na matukio 11 yapo hatua nyengine ambapo matukio sita yapo Ofisi ya Mashtaka na matukio 5 yapo mahakamani.
Nae Mratibu msaidizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkuu wa kitengo cha Takwimu za makosa ya jinai Ramadhani Himid amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao kwani vitendo hivyo hutokea sana maskuli au madrasa na kutoa tahadhari kwa wageni wasiaminiwe kabisa wanapofika mitaani.
Pia Mwenyekiti wa Mahkama ya watoto Zuweina Mohammed Abdullah amesema jamii iwe karibu na watoto kwa kuwapa elimu ili waepukane na vitendo vya udhalilishaji hasa kulawiti.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi Amina Salum Ali amefanya uzinduzi wa kitabu cha Ripoti cha viashiria vya jinsia vilivyomo katika mpango wa maendeleo endelevu (EDGS) Zanzibar.
Akitoa wito baada ya uzinduzi huo mwenyekiti huyo amesema nguvu zizidishwe kwa kuwalinda watoto na kuwaacha kwa muda mrefu bila kujua wako wapi na wanacheza na watu wa aina gani.
Pia ameomba sheria ya watoto ipitiwe upya kwa lengo la kuwarekebisha watoto kupatiwa adhabu iliyokuwa ngumu kidogo ili waweze kujirekebisha na waache kufanya vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment