RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi
wakisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege
wa Mwanza akielekea Mkoani Mara kuhudhuria maziko ya mlinzi wake Marehemu
Kagere Thomas Charles Mukakaro aliyefariki wiki hii.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimfariji na kumpa mkono wa pole Mama
Mzazi wa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro.Bi. Grace Mukakaro, baada ya
kuwasili katika Kijiji cha Nyasusura Mkoani Mara kuhudhuria maziko hayo
yaliofanyika leo 26-2-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi
wakiwafariji Watoto na familia ya
Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, baada ya kuwasili Kijijini kwao
Nyasusura Mkoani Mara, kuhudhuria maziko hayo yaliofanyika leo
VIJANA walioandaliwa kwa ajili ya kuchukua
jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro wakiwasili
katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maziko kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara
leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi
wakijumuika na Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Nyasusura Mkoani
Mara katika maziko ya marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro yaliofanyika leo
26-2-2022, kijiji kwao.
WANAFAMILIA ya Marehemu Kagere wakiongozwa na
Mama Mzazi wa Marehemi Bi Grace Mukakaro (mwenye gauni jeupe) akiwa na Watoto
wa marehemu na Mjane wa Marehemu Bi. Gladyness Tandila wa mwinsho (mwenye gauni
jeusi)
WANAFAMILIA ya Marehemu Kagere wakishirika
katika ibada maalum ya kumuombea wakati wa maziko hayo yaliofanyika kijijini
kwao nyasusura Mkoani Mara leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa salamu za pole kwa Wanafamilia na
Ndugu wa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro aliyekuwa mlinzi wake, wakati
wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022
WANANCHI wa Kijiji cha Nyasusura Mkoani Mara
wakishiriki katika Ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa maziko hayo
yaliofanyika Kijiji kwao leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitowa
heshima za mwisho kwa Marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro aliyekuwa mlinzi
wake, wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo
26-2-2022
MAMA Mzazi wa Marehemu Kagere Bi Grace Mikakaro
akitowa heshima ya mwisho kwa marehemu wakati wa maziko yaliofanyika Kijijini
kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.
MJANE wa Marehemu Kagere Bi. Gladeness Tandila
akitowa heshima ya mwisho kwa marehemu mume wake Kagere wakati wa maziko
yaliofanyika kijijini kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022, akisaidiwa na
ndugu na jamaa
WATOTO wa Marehemu na Ndugu na Jamaa wakitowa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kagere wakati wa maziko hayo
yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022
WANANDUGU wa Marehemu Kagere wakiongozwa na Mama
Mzazi wa Marehemi Bi. Grace Mukakaro akiwa na Mjane wa Marehemu Bi. Gladeness
Tandila na Mtoto wa marehemu wakiweka mchanga katika kaburi baada ya kuwekwa
mwili wa marehemu wakati wa maziko hayo yaliofanyika kijijini kwao Nyasusura
Mkoani Mara leo 26-2-2022
WATOTO wa Marehemu Kagere wakiweka mchanga
katika kaburi la baba yao wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao
Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa
mlinzi wake marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, yaliofanyika Kijijini kwao
Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kagere Thomas Charles Mukakaro, aliyekuwa mlinzi wake, baada ya kuwekwa mwili wa marehemu wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijiji kwao Nyasusura Mkoani Mara leo 26-2-2022.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment