Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Chongolo Wilayani Bariadi leo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Kikundi cha Vijana Dutwa kinachotengeneza bidhaa za ngozi, kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Mussa Nchambi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa kwenye picha ya pamoja na Kikundi cha Vijana Dutwa kinachotengeneza bidhaa za ngozi pamoja na wananchi wa jirani mara baada ya kumaliza ziara yake hapo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa shina namba 13, Tawi la Igaganulwa kata ya Dutwa, Bariadi kwenye  mkutano Mkuu wa Shina ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Simiyu.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano mkuu wa shina namba 13, Tawi la Igaganulwa kata ya Dutwa, Bariadi ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Simiyu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza mara baada ya kuonyweshwa mchoro wa mradi wa ujenzi wa eneo la biashara ndogo ndogo katika eneo linalojulikana kwa jina la soko la jioni Bariadi.
(Picha na CCM Makao Makuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.