Habari za Punde

Benki ya CRDB Yashinda Tuzo Mbili za Masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Kitaifa Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi. 
Wananchi mbalimbali waliotembelea Banda la Benki ya CRDB katika maonesho ya OSHA wakipata huduma katika banda hilo.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (wapili kulia) akiongozana na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani (kulia) wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi katika banda la Benki ya  CRDB.
Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela  (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete. 
Afisa wa Usalama na Afya mahala pa kazi wa Benki ya CRDB, Narsisa Kasinde (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete. 
Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete. 
Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pmoja na Maofisa wa Benki ya CRDB. 

Benki ya CRDB imeibuka mshindi wa tuzo mbili za masuala ya usalama na afya mahala pa kazi wakati wa kilele cha madhimisho ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo tarehe 28 April, 2022. 

Tuzo hizo za sekta bora ya fedha inayozingatia usalama na afya mahala pa kazi na ile ya utoaji huduma za kijamii (CSR) zilizotolewa na OSHA na kukabidhiwa kwa CRDB na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga maadhimisho hayo.

Maadhimisho hayo yalifanyika sambamba na Maonesho ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi ya siku tatu Yenye kaulimbiu “Kwa pamoja tushirikiane kujenga utamaduni bora wa usalama na afya mahali pa kazi” yalifunguliwa rasmi tarehe 26 April ikiwa ni utekelezaji wa sera na jitihada ya Serikali katika kuhakikisha uhamasishwaji wa Usalama na afya mahali pa kazi unatekelezwa ili kulinda afya na usalama wa wafanyakazi. 

Aidha Serikali imekuwa ikishirikiana kwa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika masuala yote yanayohusu kazi na ajira. Kwa kutambua hilo Benki ya CRDB imekuwa mdau kwa kuipa kipaumbele sera ya afya na usalama mahali pa kazi kwakushirikiana na OSHA ambao ndio wasimamizi wa mpango huo. 

Akizungumza katika maonesho hayo baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani alisema, kuongezeka kwa vifaa vya digitali na matumizi ya teknolojia kumebadilisha kabisa mazingira ya kazi hususani kuongezeka kwa vihatarishi mahali pa kazi. Uchafuzi wa mazingira kutokana na baadhi ya shughuli za uzalishaji Viwandani, Migodini na baadhi ya shughuli nyingine za binadamu umesababisha mabadiliko ya tabia nchi.
 
 “Mahitaji ya dunia yanayotokana na utandawazi yamepelekea kuwepo na idadi kubwa ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa saa nyingi kuliko kawaida na matumizi ya vifaa vya kieletroniki, hivyo kwa kulitambua hilo, Benki ya CRDB imekuwa ikilipa kipaumbela swala la afya na usalama kazini,” alisema Mutani.

Mutani amesema Benki imekuwa ikiendesha program mbalimbali kwa wafanyakzi Tanzania nzima ikiwa ni pamoja na upimaji wa afya kwa wafanyakzazi wote kila mwaka, uwepo wa siku ya Afya ya Benki ya CRDB “CRDB Bank Wellness Day” inayofanyika kwa matawi yetu yote, lakini pia kuwa na Chumba maalumu cha huduma ya kwanza, Chumba cha akina mama na watoto (Lactation Room) pamoja na uanzishwaji wa mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. 

“Mustakabali wa kazi hasa wakati nchi yetu inaendelea kujenga uchumi wa viwanda na kuelekea uchumi wa kati na ukuaji wa haraka wa teknolojia inayotumika katika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi,” alisema Mutani. 

Katika juhudi za kupambana na hali hiyo kwa sasa duniani kote msisitizo umekuwa ni kuhamasisha kazi kijani (green jobs) na viwanda vinahimizwa kupunguza hewa ukaa hali ambayo itasaidia kupunguza vihatarishi sehemu za kazi na hatimaye kupunguza madhara ya kiafya kwa wafanyakazi.  

“Muhimu sana kwa sasa kuliko wakati wowote kuanza kutambua vihatarishi vipya katika maeneo ya kazi. Kutambua vihatarishi hivyo ni hatua muhimu ya kwanza kabisa itakayopelekea kuweka mikakati ya kuzuia vihatarishi hivyo ili wafanyakazi wasipate ajali na magojwa yatokanayo na kazi,” alisema Mutani.

 Ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ni mambo ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuwa vyanzo vyake vinaweza kutambulika na kuonekana tangu mapema kama tutakuwa makini. Ili kutambua vyanzo hivyo Benki yetu ya CRDB imeona uwepo wa umuhimu wa kujenga utamaduni wa masuala ya afya na usalama mahali pa kazi miongoni mwa jamii. 

Katika kujenga utamaduni wa kuzuia vihatarishi sehemu za kazi ni wakati muafaka sasa kwa nchi yetu kuingiza masuala ya afya na usalama kazini”. Alisema Misana.

Benki ya CRDB imeshiriki maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kiwete Convation Centre, Jijini Dodoma. Maonesho  yalisimamiwa na kitengo cha  Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara cha Benki ya CRDB kilichopo Makao Makuu  - Dar es salaam na kushirikiana na wawakilishi wa Osha wa Benki ya CRDB Kanda ya Dodoma. Shughuli mbalimbali zinazohusu usalama na Afya kazini zinazosimamiwa na Benki zilionyeshwa katika Banda la Benki ya CRDB katika viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.