Habari za Punde

KUMUOMBEA DUA MAREHEMU SHEIKH THABIT KOMBO YAFANYIKA ZANZIBAR

Waziri wa Kilimo ,Umwagiliaji,Mali asili na Mifugo Shamata Shaame Khamis(wapili kushoto)akiwa katika Dua ya Kumuombea aliekua Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro-shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo katika hafla ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Baadhi ya wananchi waliohuduria katika Dua ya Kumuombea aliekua Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro-shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo katika hafla ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Waziri wa Kilimo ,Umwagiliaji,Mali asili na Mifugo Shamata Shaame KhamiS akitoa nasaha katika Dua ya Kumuombea aliekua Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro-shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo katika hafla ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na siku ya kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango mkubwa uliotolewa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar katika kuijenga nchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis katika hafla ya kumuombea Dua aliyekua Katibu wa Kwanza wa Chama cha Afro-shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo huko Chukwani Wilaya ya Magharibi B.Unguja.

Amesema Serikali imeweka Utaratibu wa kisheria wa kuwaombea Dua waasisi hao waliotangulia ili kuwathamini na kuwaombea shufaa kwa mola kutokana na juhudi walizozifanya ya kuikomboa nchi na kuleta maendeleo.

Aidha Waziri shamata amesema dhamira kuu ya kuwaombea Dua Waasisi hao ni kuwaenzi na kukumbuka michango yao na kujifunza kuwa tayari kushiriki kuijenga nchi.

Akitoa Shukurani Mwanafamilia mjukuu wa Marehemu Muhidini Muhsin Ali amesema serikali inafanya  jambo jema la kuwaombea Dua na kuwakumbuka Waasisi waliotangulia kwani wao ndio walioonyesha njia njema ya kuijenga na kuweka mshikamano na Umoja katika nchi.

Ameeleza kuwa umoja ndio nguzo muhimu katika nchi hivyo ni vyema kushikamana na kupendana katika kuijenga nchi na kuleta maendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.