Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Ndg.Shaib Ibrahim Mohammed akitembelea shamba la Vijana la mbongamboga Wilaya ya Kati Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea vikundi vya Vijana Mkoa wa Kusini Unguja.
Na.Mwandishi Wewtu.
MKURUGENZI Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Shaib Ibrahim Mohamed alisema Serikali kwa kushirikiana na shirika la umeme ZECO itahakikisha kuwatengenezea mazingira bora ambayo yatawawezesha vijana ili kujipatia kipato.
Ameyaeleza hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea wadau na vikundi mbali mbali vinavyojishughulisha katika masuala ya kilimo pamoja na uwezeshaji wa vijana huko Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema pamoja na changamoto za miundombinu ya maji na umeme lakini bado hawajakata tamaa kwani serikali inachukua jitihada na kuahidiwa kupelekewa huduma hizo
Aliwapongeza vijana kwa kubuni shughuli za kilimo ,ufugaji wa samaki katika kujiletea maendeelo ambapo serikali inaendelea kuwaunga mkono ili vijana kujikwamua na hali ya umasikini.
Akizungumzia kuhusu mradi wa pesheni alisema vijana wamepiga hatua na kuweza kuzalisha na wamekuwa na mwamko wa kuwapatia taaluma vijana wengine jinsi ya kuzalisha mapesheni hayo.
Katibu wa kikundi cha ushirika umbuji famili Abdulghani Choum Khamis alisema wameamua kufanya shughuli za kilimo kwa lengo la kujikwamua kimaisha na kusaidia familia zao katika masuala ya elimu.
Katika ziara hiyo maeneo yaliyotembelewa ikiwemo kikundi cha ushirika Koani, Chuo cha maendeleo Dunga kikundi cha ushirika Bambi, Pagali,kikundi cha ushirika Umbuji famili, pamoja na Dunga kibweni.
No comments:
Post a Comment