Habari za Punde

Nilivyomfahamu Askofu Munga

 

Na.Adeladius Makwega-DODOMA

Katika matini yangu ya Mti wa Matambiko niliwataja watu watatu ambao walikuwa marafiki wa Rais wa Awamu ya Tatu Wilayani Lushoto Brigedia Hassani Ngwilizi, Karim Mahanyu ambaye alikuwa diwani wa kata ya Lukozi na Baba Askofu Mstaafu Stepheren Munga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

Kati ya marafiki hao watatu aliye hai kati ya hao mtu mmoja naye ni Baba Askofu Mstaafu  Munga, binafsi nilimfahamu tangu mwaka 2009 lakini nilikuwa naye mbali mno kati aya mwaka 2016-2018 nikiwa kwa Wasambaa wilayani Lushoto Tanga nikamfahamu kwa karibu katika shughuli za maendeleo.

Ujirani wangu na yeye ulichagizwa na mwanahabari Josephy Kweka ambaye nadhani alikuwa mtoto wa Askofu Kweka ambaye aliweka hamira ya ukaribu huo wakati akikamilisha mradi wa Redio Utume FM ambayo ulichukua karibu miaka 5 kukamilika.

Ndugu Kwema ambaye nilimaliza naye Shahada ya Sanaa ya Habari Tumaini Iringa mwka 2008 alikuwa mahiri kwenye masuala ya Redio na Runinga kw ahiyo Dayosisi Kaskazini Mashariki walimkabidhi mradi huo na akaukamilisha 2016 wakati mimi naingia Lushoto.

Huyu jamaa alikuwa na ujuzi wa kusanifu sauti na hata picha za video tangu wakati huo lakini nadhania hakuvutiwa kufanya kazi ya serikali wala taasisi zingine zaidi ya kanisa wakati huo.

Nyuma ya pazia Chuo cha Tumaini Iringa kilikuwa mali ya KKKT nadhania baadahi ya wahadhiri waliwapa Dayosisis ya Kaskazini Mashariki ndugu Kwekwa kwa kuwa alitambua uwezo wake wa kufanya kazi ya vitendoi katika redio na runinga. Nikiwa Lushoto nilibaini hata wajumbe wa Bodi wa Redio Utume FM walikuwa wahadhiri wa Chuo Kkuu cha Tumaini Iringa wakati huo mathalani Dkt Gaspaer Mpehongwa (nadhani sasa ni Profesa)

Nafika Lushoto 2016 Kweka akanitambulisha akawaambia Makwega nimesoma naye atafanya kazi nanyinyi vizuri sana, wale vijana wakanipokea tukaanza kufanya nao kazi kwa karibu mno.

Ukiachana na kufanya kazi na redio kadhaa, kun akitu kimojaliniwahi kujifunza taasisi yoyote haiwezi kufanikiwa kama kitashindwa kufanya kazi na redio kwa kuwa redio bado ni chombo chenye wasikilizaji wengi kuliko chochote ulimwenenguni. Hauwezi kufanya Propangada Fide bila redio. Ndiyo maana BBC, VOA na DW-KISWAHILI mpaka kesho bado wameyashirikilia nga nga nga matangazo yao ya redio kwa mtindo ule ule hata kama wanabadilisha viashiria vyao.

Kwa mfano ukiingia Facebook, Instragrme nahata whasaap unayasikiliza matangazo ya DW KISWAHILI. Tena ni bira kw akuwa kama muda yalipokuwa ynarushwa hukuyasikiliza utayakuta yanakungoja kwa muda wako.Wakati zamani yalikuwa yale ya Masafa Mafupi (Short Wave-SW).

Kwa wale wlaiosma mapinduzi ya CUBA ya akina Fideli Castro, Raul Castro na Che Guvera. Huyu Che Guvera alitengeza Redio ya Msituni ambayo ilitumika kurusha matangazo ya propadanda zao juu ya vita hadi mapinduzi hayo huku wanapigana msituni.Ilitwa RADIO MUDUALE.

Japokuwa kwa sasa kuna kasumba ya Runinga lakini nakwambia watu wanaotazama TV ni wachache mnona ndiyo maana DW KISWAHILI wanatumia kwa karibu redio jamii kuliko hata redio la mataifa husika zinavyozitumia redio hizo.

Mathalani wajerumnai wkaibadilisha Kansela wao leo kesho yake Afrika Mashariki nzima wanalitambua hata kulitaja jina la ndugu huyu wakati hata majina ya mawaziri wa mataifa yetu mengine hayafahamiki kabisa.

Kipindi hiki ndipo nilipokutana kwa karibu na Baba Askofu Munga.

Siku moja aliniita ofisini tukazungumza mengi sana, machache ni haya akasema katika jamii kufanya kazi ni muhimu sana kama kiongozi–hilo wajibu wako lakini jamii unayoingoza kutambua kazi unayoifanya hilo ni jukumu ya jamii yako unayoiongoza, akasema siyo serikalini hata kwenye taasisi za dini huku tulipo sisi.

Fanya kazi itakuwa ushuhuda kwao kama si leo basi kesho. Baba Askofu alipomaliza maneno hayo akasema tusali mimi nikapiga magoti yeye akasimama akaomba, alipomaliza akaniruhusu niende zangu kuendelea na majukumu.

Redio hii tulitumia mno huku tukiwapa haki yao na wao wakifanya kazi hiyo kwa moyo na nguvu zao zote. Wakati tunaendelea na kazi nikabaini hata Mzee Mkapa walikuwa wanaelewana naye mno.

Wakati huo wilaya ya lushoto ilikuwa inafanya vibaya kitaaluma nadhani mwaka 2017 shule tatu za mwisho kitaifa kwa misingi zilitoka huko ikiwamo Mhinduro ambayo ilikuwa kata ya Mbaramo.

Kazi hii kwa karibu tuliifanya na watu wawili Elizabeth Msoka (Mchaga) Muhsini Magogo (Msambaa) hawa walikuwa wanaweza sana kuhamasisha jamii hii ya Kisambaa Msoka alikuwa Bibi Mifugo na Magogo alikuwa Mwalimu

Hawa ndugu wakapanga mpango wa namna tukavyofanya kazi hiyo vijijini ikiwamo kata ya Lunguza, Shagayu, Mtae na Mbaramo kuhamasisha kazi za maendeleo. Tukaweka kambi huku tukitoa mbuzi bora, kuku na hata mshine za kumwagilia na huku tukisisitiza umuhimu wa chakula cha mchana shuleni.

Huku Lunguza na Mbaramo tuliwasiliana na viongozi wa kanisa la KKKT wkaweka maizngira vizuri na Waisilamu kwa bahati nzuri diwamni Mbaramo alikuwa ni Imamu wa Msikiti wa Ijumaa katika Kijiji hicho.

Aliamka mama Msoka (mchaga) aliajiliwa na hii halmashauri akiwa binti mdogo sana kw ahiyo alipofika Lushoto aliweza kuwa sehemu ya jamii hii kw ahiyo alikw anazungunza Kipare , Kisambaa na hata Kimbugu kwa kiasa.

Akaanzisha wimbo Kisambaa wa hamasa.

“Mbaramo hodi hodi…Mmgeni akiingia mpokee, mgeni akingia mpokee…” huku akiyataja majina ya waliopo.

Alisimama Mhusini Magogo (Msambaa) akayasema maneno haya kwa Kisambaa

Jamani watu wa Mbaramo Shekhe Ulanga ambaye ni Diwani haiwezi kuwa ni imamu wa milele, ipo siku nguvu zake zitapungua, kwa hivi sasa mna jukumu la kumuanda kijana mwingine ili awe imamu wetu, ili muwe na imamu huyo matamchukua mtu yoyote tu? Wakajibu hapana, Kwani lazima awe anasoma dini na kuielewa, kama Sheikh Ulanga au zaidi yake.Ka hiyo jamani tupeleke watoto shuleni kwa kuwapa mahitaji yote muhimu ikiwamo chakula cha mchana.

Mama msoka akaingia tena na wimbo Kisambaa nikakaribishwa mie mwanakwetu.

Nikawasalimu nikawaambia mie jina langu la ukoo naitwa Makwega ni jina la Kipogoro likimaanisha KUKWEGA maana yake kuvuta kitu, hapa nipo mbele kuwavuta katika maendeleo. Nikaawaambia nyinyi maendeleo mnayo nyumba zenu zote za bati, msikiini yot nadhifu nahata makanisa yenu mazuri sijaona kanisa la nyasi (wakacheka)

Nilipokuwa nakuja nimejulishwa kuwa Askofu Munga alizaliwa Tewe Lunguza lakini alisoma shule ya Msingi Mbaramo hapa kwenu kwa kuwa wakati huo Tewe hawakuwa na na shule ya msingi, baadaye akasomba Maramba, Tambaza sekondari hadi vyuo vikuu na sasa anaongoza kanisa Dayosisi yenu.

Nikauliza kasoma hajasoma, wakajibu kasoma.

Ebu tazameni umbali wa Tewe na Mbaramo lakini ndugu yenu huyu alisoma na akahitimu maana yake alitembea kwa mguu.

Sasa watoto waende shule lakini tuwape watoto wetu chakula cha mchana kwa utaraibu mtakopanga wenyewe na viongzo wenu wa vijiji kwa maana nimekuja hapa shule yenu moja imekuwa ya mwisho kitaifa si tunamti aiabu baba Askofu?

Wakajibu ndiyo. Tulimaliza mkutano na Kurudi zetu Lushoto na yote tuliokubaliana nayo yalitekelezwa ipasavyo.

Hawa ndugu zake Baba Askofu Munga hawakuwa tena wa mwisho kitaifa walijitahidi. Sifahamu kwa sasa.

Mwanakwetu naomba niweke kalamu yangu chini kwa kukuuliza maswali kadhaa Je hapo ulipo kuna kiongozi gani mwenye jina kubwa iwe kikata kiwilaya au kitaiafa? Je mmemtumia vipi kuhamisisha maendeleo ya eneo lenu? Changamkieni tumieni hilo jina  kuhamasisha hata watoto wenu wale chakula cha mchana shuleni ili kuongeza uelewa na ufaulu.

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.