Habari za Punde

Gaudentia Kabaka Awapongeza UWT Iringa Kwa Ujenzi wa Nyumba za Makatibu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudentia kabaka akiwa na zawadi ya kikombe cha chai chenye picha yake ambayo hubarika kila wakati kikiwa na chai kinatokea picha yake kisipokuwa na chai kinakuwa cheusi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudentia kabaka akipokea tuzo ya uongozi bora kutoa kwa viongozi wa UWT Iringa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudentia kabaka akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali wa serikali na chama wakati wa ziara yake mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudentia kabaka   amewapomgeza UWT mkoa wa Iringa kwa ujenzi wa nyumba za makatibu na kukiimarisha chama na kuongeza ushirikiano baina ya serikali na chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili mkoani Iringa,Kabaka alisema kuwa uongozi wa umoja huo umefanikisha kukituliza chama cha mapinduzi kutokana na utulivu uliopo kwenye jumuiya hiyo.

Kabaka alisema kuwa viongozi wa UWT mkoa wa Iringa wamekuwa viongozi imara katika kuiongoza jumuiya hiyo ndio maana wamekuwa na umoja na mshikamano katika uongozi.

Alisema kuwa kwa mara ya kwanza miaka mitano ya uongozi wake amefanikisha kuongeza idadi ya wabunge wa viti maalum kuwa wengi bungeni.

Kabaka alisema kuwa sasa ni wakati sahihi wa kuchagua viongozi ambao wataweza kuiongoza jumuiya hiyo na kuendelea kuwa imara kwa ustawi wa chama cha mapinduzi.

Alisema kuwa wanawake wote wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo wachukue fomu na wagombee kwa ajili ya kuingoza na kuikuza jumuiya hiyo.

Kabaka alisema kuwa chama cha mapinduzi kinautaratibu mzuri wa kuwachuja viongozi wanaotaka kugombea hivyo amewataka kuondoa wasisi wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya UWT

Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka amewashukuru kabila la wahehe kwa kumvisha nguo za kihehe ambazo zimemuongezea heshima kubwa katika uongozi wake.

Alisema kuwa amefurahi kuvishwa vazi hilo ambalo kwa miaka mingi amekuwa anaona kwenye tv tu historia ya chief mkwawa hivyo ameahidi hata livua vazi hilo hadi amalize ziara mkoa wa Iringa na ataendelea kulivaa mara kwa mara.

Lakini pia mwenyekiti wa UWT Taifa aliwashukuru UWT mkoa wa Iringa kwa tuzo na zawadi mbalimbali ambazo amepewa leo mkoa wa Iringa kuwa hatawasahau wema wao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa,Niocolina Lulandala alisema kuwa wanampongeza mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka  kwa kuijenga ofisi ya UWT ambayo idara zote za jumuiya hiyo zinapatikana makao makuu ya chama jijini Dodoma hivyo kwa miaka yake mitano amefanya maendeleo makubwa kwenye umoja huo.

Lulandala alisema kuwa mwenyekiti wa umoja huo amefanikiwa kuunganisha jumuiya ya UWT kuwa na umoja na ushirikiano ambao umesadia kuongeza wananchi chama wapya na kukisaidia chama kufanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali za utawala.

Alisema kuwa wameendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi wa jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa ambazo zitawasaidia kuacha kupanga mtaani zote hizo kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka katika kuhakikisha watumishi wote wanaishi kwenye nyumba zao

Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudentia kabaka amekabidhiwa tuzo ya umahiri katika kuiongoza jumuiya ya UWT taifa kwa kuiwezesha jumuiya hiyo kuwa na umoja na ushirikiano katika kukikuza chama cha mapinduzi.

Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM Iringa wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na serikali ndio maana mkoa wa Iringa umetulia na unafanya kazi za kimaendeleo.

Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa umetoa zaidi ya bilioni kwenye mfuko wa akina mama wa asilimia 4 na wamejipanga kuhakikisha mwaka ujao wa fedha wataongeza zaidi ya hapo.

Sendiga alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuwatua ndoo wanawake wa mkoa wa Iringa kwa kuleta miradi mingi ya maji kila wilaya na halmashauri zake.

Alisema kuwa Iringa bado kunachamoto ya ukatili wa kijinsia hivyo serikali ya mkoa wa Iringa imeanza kuwafunga watu wote ambao wamekuwa wanafanya vitendo vya kikatilii.

Sendiga alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa waache mara moja tabia ya kuwaficha wananchi ambao wamekuwa walifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili serikali ichukue hatua stahiki kwa watuhumiwa hao.

Mwenyekiti wa cham cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Dkt Abel Nyamahanga alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga amekuwa kiongozi bora kuiongoza Iringa kuleta maendeleo ya wananchi.

Dkt Nyamahanga alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimemteua mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendinga kuwa balozi wa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa.

Aidha Dkt Nyamahanga alisema kuwa wanachama wote wa CCM mkoa wa Iringa wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho bila uoga wowote ule.

Alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa itawachukulia hatua kali watu wote ambao wameanza kampeni mapema na wale ambao wamekuwa wakitoa na kupokea rushwa ili wapate uongozi.

Nyamahanga alisema kuwa Iringa wataendelea kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kila jambo ambalo amekuwa akilifanya kuleta maendeleo kwa watanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.