Habari za Punde

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFANYA TAFRIJA KUWAAGA WASTAAFU WAKE

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Chritopher Kadio (Kulia), akipokea zawadi ya picha inayomuonyesha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru ndani ya Jahazi kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Baraza Mvano (Katikati) ambaye ndiye Mchoraji wa Picha hiyo. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo John W. Masunga akishuhudia makabidhiano hayo. Picha hiyo ni Zawadi Maalum kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mstaafu huyo.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji leo usiku wa tarehe 18 Juni, 2022 limefanya tafrija fupi ya kuwaaga watumishi wake waliomaliza muda wao wa Utumishi ndani ya Jeshi hilo na kula chakula cha pamoja kama ishara ya Upendo.

Tafrija hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma, ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemoKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa shughuli hiyo.

Waliowakilisha wenzao na kupongezwa kwa Utumishi bora ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji usiku huo ni pamoja na Naibu Kamishna Mstaafu Fikiri Salla, Kamishna Msaidizi Mstaafu Baraza Mvano, Kamishna Msaidizi Mstaafu Bakari Mrisho, Ndg. Rajabu Mfyome, Ndg. Felis Mshana na Bi. Evelyne Kadiva.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliwataka wastaafu kutumia kwa uangalifu viinua mgongo vyao watakavyovipata kwani ni kipindi ambacho kila mtu hutolea macho kwa nia ya kuhitaji msaada.

Naye Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga aliwashukuru wote waliomaliza muda wao wa Kiutumishi ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kuwatakia heri katika maisha yao ya ustaafu.

Tafrija hiyo ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje Mheshimiwa Vita Kawawa (Mb) Makamishna, Viongozi Waaandamizi, Maafisa, Askari na Watumishi wa kada ya kiraia wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Dodoma 18 Juni, 2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.