Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe, Masoud Ali Mohammed amewataka mafundi kuwa wazalendo katika ujenzi kwa kuzingatia viwango ili kupata majengo yenye ubora nchini.
Akiwa katika ziara ya kukagua majengo ya kikosi cha Valantia amesema amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo kuona unaenda vizuri ambao unajumuisha nyumba za wakuu wa kambi, ofisi, mahanga ya wapiganaji pamoja na nyumba za kuishi wapiganaji wa kikosi hicho.
Amesema kuwa ili majengo yawe imara lazima kuzingatia ubora wa vifa vya ujenzi pamoja na kujali muda uliyopangiwa kukamilika hivyo kasi ya ujenzi huo inatarajiwa kukamilika kwa muda mfupi.
Aidha amefahamisha kuwa ingawa jengo linalojengwa katika eneo la kikungwi litakua na nyumba ya Mkuu wa wa Kambi hiyo ,pia litakuwa na makao makuu ya kambi ili wapiganaji waweze kuishi.
Waziri ameongeza kusema kuwa licha ya kuwepo kwa majengo ya ofisi pia wapiganaji wana haki ya kujenga kila wanachohisi muhimu kujengwa katika eneo hilo ili kurahisisha huduma muhimu zinazohitajika.
Aidha Waziri huyo amemtaka Enginear anaesimsmamia ujenzi huo kuhakikisha ujenzi unakuwa na kiwango na kukamilika kwa wakati.
Nae Mkuu wa Kikosi cha Valantia Luten Kanal Saidi Ali Shamhuna amesema vifaa vyote vya ujenzi vipo hivyo wanaendelea kujenga na kuhakiksha kuwa ujenzi huo.
Ziara hiyo imejumuisha kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Muyuni C’Kikungwi, Mto wa maji na Mwanyanya ambapo katika eneo hilo wameomba kupatiwa barabara.
No comments:
Post a Comment