Habari za Punde

Jeshi la Zimamoto Lapokea Ugeni Kutoka Jiji la Hamburg

Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, DCF Charo Mangare akisoma taarifa yake, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya kupokea ugeni kutoka Jiji la hamburg nchini Ujerumani, katika Maadhimisho ya sherehe ya miaka 12 ya ushirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann akilishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kusimamia vema vitendea kazi na mafunzo wanayowapatia kwa kipindi cha miaka 12 ya mashirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi wakionesha umahiri wao mbele ya ugeni toka Jiji la Hamburg jinsi ya kufanya uokoaji kwenye majengo marefu pindi madhara yanapotokea wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Maafisa, Askari na Wageni mbalimbali walioshiriki katika Maadhimisho ya sherehe ya miaka 12 ya mashirikiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, hafla iliyofanyika leo Julai 2, 2022 katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Nyanda, akitoa maelezo mbele ya ujumbe toka Jiji la Hamburg, vifaa vya msaada walivyopatiwa na Jiji hilo vinavyolisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kutekeleza majukumu yake, wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam

Katibu wa Mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann (katikati), Kaimu Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (DCF) Charo Mangare (Wapili kushoto), Mratibu wa Uhusiano kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg Bi.  Inken Bruns (Wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Uokoaji Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (DCF) Bashiri Madhehebi (kulia), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo pamoja na ujumbe toka Jiji la Hamburg wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam leo Julai 2, 2022.

 (PICHA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.