Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi Atoa Mkono wa Eid Al Hajj Kwa Wazee

MSAHAURI WA RAIS masuala ya Siasa Mhe.Ali Salum Haji (Kirova)  alipokuwa akitoa salamu kwa niaba ya Mke wa Rais Mama Marium Mwinyi wakati wa kutoa mkono wa Idd  El Hajj kwa wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Mjini Magharibi ikiwa ni utaratibu wake Mke wa Rais kila ifikapo Kipindi cha Sikukuu  kwa   Wazee hao.

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi  Mama Mariam Mwinyi amewataka watoto wanaolelewa katika vituo mbali mbali nchini kuwa makini na waangalifu wakati wanapokwenda na kurudi katika viwanja vya sikukuu, ili kuepukana na changamoto mbali mbali zinazoweza kuwakuta.

Mama Mariam ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya ‘Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) ’ ametoa wito huo kwa nyakati tofauti alipotembea vituo mbali mbali vinavyotunza na kulea watoto  na kuwakabidhi zawadi za mkono wa Idd el Hajj.

Katika hafla hiyo mama Mariamu aliwakilishwa na Mtendaji Mkuu wa ZMBF Mwanaidi Mohamed Ali, ambapo alitembelea vituo vya ZASO Children Home kiliopo Founi Mambosasa, Kituo cha SOS pamoja na Kituo cha Kulelea watoto Mazizini, Mkoa Mjini Magharibi.  

Alisema kuna umuhimu mkubwa kwa watoto hao kujilinda wakati wote wanapokwenda na kurudi kwenye viwanja  vya sikukuu, huku  akiwataka watoto wenye umri mkubwa kubeba dhima ya  uangalizi kwa wale wenye umri mdogo, ili waweze kukamilisha sikukuu hiyo wakiwa salama na wazima.

Aidha, aliwatakia kheri nyingi watoto hao katika sikukuu hiyo na kusisitiza umuhimu wa kutimiza jukumu lao la kuwatii wazazi na walezi pamoja na kusoma kwa bidii.

Nae, Mkurugenzi wa Idara ya ustawi wa Ustawi wa Jamii na Wazee Abdalla Saleh Omar aliwataka watoto hao kufuata maelekezo wanayopewa na walezi wao, sambamba   na kujikinga na vishawishi vyote ili waweze kufanikiwa.

Aliwakumbusha watoto hao wajibu walionao wa kuongeza bidii katika masomo yao, akibainisha hatua hiyo itawawezesha kufikia mafanikio makubwa katika siku za usoni.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya nane itaendelea kuwahudumia kikamilifu watoto wote nchini, ikiwa ni hatua ya kuendeleza utaratibu ulioasisiwa na Awamu ya kwanza ya Serikali  mara baada ya Mapinduzi ya 1964.

Mkurugenzi huyo alisema kipindi hicho cha sikukuu  ni wakati wa furaha kwa watoto wote, hivyo akawataka kuthamini viongozi wa Maisha Bora Foundation, chini ya Uongozi wa Mama Mariamu kwa kufika vituoni humo na kutoa mkono wa Idd el Hajj.

Aidha, Viongozi wa Vituo hivyo wamemtakia kheri na Idd njema Mama Mariamu na familia yake na kutoa shukrani za dhati  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kwa namna wanavyowapenda, kuwajali na  kutetea maslahi ya watoto nchini kote.

Vile vile, mtoto Rauhiya Omar Ali kutoka kituo cha ZASO akitoa neno la shukrani, alimuomba Mwenyezi Mungu kumjaalia afya bora na maisha mema Mama Mariamu kwa kuwajali na kuwathamini watoto, sambamba na msaada wake uliofanikisha kituo hicho kupata leseni.

Katika hatua nyengine, wazee wanaoishi katika Vituo vya kutunza wazee vya Sebleni na Welezo nao walipatiwa zawadi hiyo ya mkono wa Eid Hajj.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

Wazee wanaoishi Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini  wakisikiliza kwa makini salamu za Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi (hayupo pichani) zilizotolewa kwa niaba yake na mshauri wa Rais Siasa  Mhe.Ali Salum Haji (Kirova)   wakati wa  Utoaji wa mkono wa Idd    kwa wazee hao leo.
Afisa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Rais Ikulu Khadija Pembe Juma akitoa Mkono wa Idd el Hajj kama  Sikuu ya Wazee wanaoishi nyumba za Wazee  Sebleni kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi,ambapo ni utaratibu wake kila ifikapo kipindi k ichi kipindi cha Sikukuu kwa Wazee hao.
Wazee kinamama na Kinababa wanaoishi katika Nyumba za Wazee Sebleni wakiitikia dua iliyoombwa  mara kupokea mkono wa Idd El HaJJ   ikiwa ni sikukuu yao iliyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi, hafla iliyofanyika leo katika makazi yao Sebleni Wilaya ya Mjini.
[Picha na Ikulu] 10 julai 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.