Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Awapongeza Wachezaji wa Serengeti Girls Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) pamoja na viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla aliyowaandalia wachezaji wa Timu hiyo kuwapongeza baada ya kufuzu kombe la Dunia la Vijana litakalofanyika nchini India.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa,Katibu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Wallace Karia katika picha ya Pamoja na Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) kabla ya hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

                                                                          Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.