Habari za Punde

BENKI ya CRDB Yakabidhi Ngombe wa Maziwa Watano kwa Kikundi cha Manyame Sasa cha Ufugaji.

Watendaji wa Benki ya CRDB wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kutembelea banda lao la Maonesho katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo na kukabidhi Ngombe Watano wa Maziwa kwa Kikundi cha Wajasiriamali cha Manyame Sasa, Ngombe hao wametolewa na Benki ya CRDB kwa Mkopo kwa Wajasiriamali wa Kikundi hicho. 


Meneja Mahusiano,Kilimo, Biashara wa Benki ya CRDB Ronald Melkiori  akitowa  maelezo ya huduma za Benki ya CRDB wanazozitoa kwa Wateja katika sekta ya Kilimo Nchini, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alipotembelea Banda la Maonesho la Benki ya CRDB katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo 8-8-2022, baada ya kuyafungua na kutembelea Maonesho hayo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati Bw. Badru Iddi akitowa maelezo ya wakati wa kukabidhi Mkopo wa Ngombe kwa Kikundi cha Wajasiriamali cha Manyame SASA, wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja. Kikundi hicho kimekabidhiwa Ngombe Watano wa Maziwa kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya CRDB. 
Ngombe wa Maziwa Watano waliokabidhi Kikundi cha Wajasiriamali cha Manyame Sasa kutoka Benki ya CRDB kwa mkopo nafuu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati Bw. Badru Iddi akitowa maelezo ya wakati wa kukabidhi Mkopo wa Ngombe kwa Kikundi cha Wajasiriamali cha Manyame SASA, wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja. Kikundi hicho kimekabidhiwa Ngombe Watano wa Maziwa kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya CRDB.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Ngombe Watano wa Maziwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Manyame Sasa Bi. Rukia Abdalla Mwinyi waliotolewa Mkopo na Benki ya CRDB. na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana. 

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Mwanyame Sasa kinachojishughulisha na Ufungaji Bi. Rukia Abdalla Mwinyi akizungumza na kutowa shukrani kwa Benki ya CRDB kwa mkopo wa Ngombe wa maziwa watano waliokabidhi leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane.

Wanakikundi cha Ufugaji cha Manyame Sasa wakiwa na Ngombe wao wa Maziwa Waliokabidhiwa Mkopo kupitia Benki ya CRDB, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo 8-8-2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.