Habari za Punde

Maofisa wa Benki ya NMB Washiriki Amref Wogging Marathon Zanzibar. Kilomita 10 na Kilomita 5." Kuchangia "Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama"

Maofisa wa Benki ya NMB wakishiriki katika matembezi ya Amref Wogging Marathon ya kilomita 10 na Kilomita 5 yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Maisara Suleiman na kumalizika katika viwanja vya Amaan Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2022 yalioandaliwa na Amref Tanzania kwa kuchangia Vifaa Tiba kwa Usazi Salama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha Uchangiaji wa Fedha kwa ajili ya Kuchangia VifaaTiba kwa Uzazi Salama Ofisa wa Benki ya NMB, baada ya kumalizika kwa matembezi ya Amref Wogging Marathon, yalioazia katika viwanja vya Maisara Suleiman na kumalizikia katika viwanja vya Amaan Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
Timu ya Maofisa na Wakuu wa Benki ya NMB walioshiriki Amref Wogging Marathon wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo katika viwanja vya Amaan leo.Wakuu wa Benki ya NMB wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika viwanja vya Amaan Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa matembezi ya Amref Wogging Marathin yalioazia katika viwanja vya Maisara Suleiman na kumalizikia  uwanja wa Amaan. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.