Habari za Punde

Serikali ya Ujerumani imekusudia kuanzisha mfuko wa bima ya Afya (Health Insurance)

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Wabunge wa Chama cha Social Democratic Part  cha Ujerumani  walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja  kutaka mashirikiano katika mambo mbalimbali ya Maendeleo ya Afya 
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Wabunge wa Chama cha Social Democratic Part  cha Ujerumani  walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja  kutaka mashirikiano katika mambo mbalimbali ya Maendeleo ya Afya 
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (KULIA) akimkabidhi zawadi maalum Mbunge wa Chama cha Social Democratic Part  cha Ujerumani Tina Rudolph wakati alipofika Ofisini kwake Mnazimmoja kuendeleza mashirikiano   Kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ujerumani .PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.17/8/2022

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazurui Amesema kuwa Serikali ya Ujerumani imekusudia kuanzisha mfuko wa bima ya Afya (Health Insuarence)   ambao utasaidia wananchi kuwapunguzia gharama za matibabu na kuweza  kupata huduma bora Nchini .

 Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazimmoja wakati alipotembelewa na  wabunge wa chama cha Social Democratic Part cha Ujerumani   kujadili namna  ya kupunguza na kumaliza  maradhi mbalimbali ikiwemo  Kifua Kikuu,HIV,Homa ya Ini na Malaria.

Amesema kuwa ni muhimu sana kutumia bima kwani kutasaidia kuinua hali za wanyonge ambao hawawezi kumudu gharama kubwa za matibabu hivyo  kutawezesha kupunguza ugumu wa gharama za matibabu kwa wananchi wa Zanzibar.

Aidha  Mhe.Mazrui  amefahamisha kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Zanzibar na Serikali  ya Ujerumani unazidi kuimarisha sekta ya Afya Nchini kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa katika  kupunguza maradhi mabalimbali.

“  ujio wa Wabunge  hawa utaimarisha mashirikano kati yetu  na Wajerumani na   utasaidia zaidi kuimarisha Sekta ya Afya katika kukabiliana na Maradhi mbalimbali, endapo tutauzinduwa mfuko huu utatuinua kimatibabu  kwani Wananchi wengi hatumudu gharama kubwa  za matibabu”.alisema Waziri huyo.

Hata hivyo Waziri Mazrui amewahakikishia wabunge hao kuwa msaada wao wanaoutoa  unatumika vizuri  katika kuimarisha matibabu kwa kununua vifaa tiba ambavyo vinasaidia wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

Nao wabunge  hao wameahidi kuendeleza ushirikiano wao kwa lengo la kustawisha afya za wananchi wote wa Zanzibar.

Tokea 2002 Ujerumani imeanzisha ushirikiano na Zanzibar ambapo ilianzisha mfuko wa( Global Fund)  unaosaidia   kupambana na maradhi mbalimbali Nchini. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.