Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Mwanakhamis Adam Ameir amesema suala la kuwapatia elimu watoto ni jukumu la wazazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ili taifa liweze kupata wataalum wa baadae.
Akifungua mkutano wa kupanga mikakati ya kuwasaidia watoto kurudi Skuli kwa Polisi jamii wa Wilaya ya Magharibi B katika ukumbi wa Aboud Jumbe Mwinyi huko fuoni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja amesema elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto hivyo wazazi nao wanapaswa kuwasimamia ili kuipata haki hiyo.
Amesema Wizara ya Elimu kupitia mradi wa kuwarejesha watoto Skuli walio na umri wa miaka Saba Hadi 14 watahakikisha wanatumia mikakati madhbuti ili watoto hao wafanikishe ndoto za maisha yao.
Aidha Dkt Mwanakhamis amewaomba Polisi Jamii hayo kupanga mikakati itakayosaidia kuapatina watoto hao katika maeneo yote ya shehia zao.
Kwa upande wake mkurugenzi idara ya Elimu mbadala na watu wazima bi mashavu Ahmada fakih amesema kwa hatua ya awali Wizara kwa kushirikiana na jamii kupituia mradi huo tayar wameweza kurejesha zaidi ya Wanafunzi elfu10 hivyo Bado jitihada zinahitajika ili kuliondosha kabisa tatizo ilo Katika jamii zao.
Nae Mratibu wa Mradi wakuwarejesha watoto Skuli Bw Mzee Shiraz Hassan amesema katika kuwahamasisha watoto kurudi Skuli na kubaki madarasani ni pamoja na kuwapatia sare za Skuli na vifaa vya kujifundishia kwa lengo la kuwapa hamasa ya kuendelea na masomo.
Kwa upande wao Polisi Jamii hao wamesema ili kuwasaidia na kuwaondosha wimbi la watoto walioacha masomo katika mikakati yao ni kuondoshwa michezo ya gemu katika mitaa ambazo zinachangia kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto watoro.
No comments:
Post a Comment