Habari za Punde

SMZ Yampongeza Mwanamichezo Nassor Salum Ali (Nassor Mahroq) Kwa Kushiriki Vyema Mashindano ya Jahazi Duniani.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Saim akimzawadia zawadi ya Jahazi ya Mtembe Nassor Salum Ali Mahroq (kulia kwake) kwa kushiriki vyema na kumaliza mashindano ya Kutweka kuwa Mzanzibar wa kwanza kushiriki mashindano hayo yanayohusisha kuzunguka Dunia kwa kutumia Jahazi zisizo kuwa na mashine,hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja na kulia kwake) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mhe. Ibrahim Bhaloo.   
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said wakati akimpatia cheti cha shukurani Bw.Nassor Salum Ali Mahrouk katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya kumpongeza kwa mchango wake katika kuvitangaza visiwa vya Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hapo

"Wahenga wanasema mcheza kwao hutunzwa..Hivyo basi kwa kuliona hili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupitia Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imeamua kutumia fursa hii kumpongeza Bwana Nassor sio tu kwa kuwa mzanzibari wa kwanza kushiriki mashindano haya maarufu duniani ila pia kwa kutokuchoka kwake kuvitangazia visiwa vya Zanzibar kwa muda wote aliopata nafasi ya kufanya hivyo"

Hayo aliyasema Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said wakati akimpatia cheti cha shukurani pamoja na zawadi ya mtepe(Jahazi) Bw.Nassor Salum Ali Mahrouk katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya kumpongeza kwa mchango wake katika kuvitangaza visiwa vya Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hapo Mnazimoja leo tarehe 16/08/2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.