Habari za Punde

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAAZI KWA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA TAREHE 19/08/2022.

Ndugu Waandishi wa Habari

UTANGULIZI.

Kufuatia uzinduzi wa zoezi la ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAAZI  uliofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi alioufanya tarehe 8/4/2022 katika ukumbi wa hoteli ya GOLDEN TULIP, ambapo alizindua Nembo na tarehe ya kufanya ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAAZI kwa lengo la kuanza matayarisho ya Sensa hiyo hapo 23 August 2022.

Ndugu Waandishi wa Habari

Katika kutekeleza zoezi la sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja imejipanga kutekeleza zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa kupitia Kamati za Sensa za Mkoa, Wilaya na  Shehia, sambamba na kushirikisha viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na makundi mengine ya kijamii kwalengo ka kuwafikia zaidi wananchi na i katika kuhamasisha kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia serikali kupanga mipango ya maendeleeo kwa kipindi cha miaka kumi ijayo kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi ngazi ya shehia.

Ndugu Waandishi wa Habari

Mkoa ulizindua mafunzo kwa makarani wa sense ya watu na makaazi  tarehe 31/7/2022 katika vituo vinne ikiwemo kituo cha mahonda, Fujoni, Mkokotoni na Mkwajuni ambapo jumla ya makarani 967 wamepatiwa mafunzo kwa muda wa siku 19 wakiwemo Makarani wa kawaida 817, maafisa TEHAMA 75 na Maafisa maudhui 75.

Makarani hawa ndio watakaokuwa mstari wa mbele katika kukusanya taarifa za kaya na taarifa za kijamii, hivyo nawaomba sana wananchi wa Mkoa wa Kasakzini wenzangu kuwapokea na kuwapa mashirikiano ili waweze kutimiza jukumu lao hili kubwa walilopewa na taifa kwa manufaa yetu na Taifa letu.

UTEKELEZAJI.

Ndugu Waandishi wa Habari

Katika kukusanya taarifa za ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAAZI Mkoa  unalenga kuhakikisha wananchi wote wanahesabiwa tena mara moja tu kwa kila mtu. Zoezi la kuhesabu watu litaanza tarehe 21/08/2022 kwa kukusanya taarifa za kijamii kupitia dodoso la jamii ambalo litakwenda kukusanya taarifa zote za huduma za kijamii zilizopo katika shehia na zile ambazo hazimo katika shehia kwa lengo la kupima na kuelewa huduma ambazo wananchi wanazihitajia kwa kipindi cha miaka kumi ijayo na serikali kuweza kupanga mipango yake katika kuwapelekea huduma hizo wananchi katika ngazi ya shehia.

Ndugu Waandishi wa Habari

Baada ya kukamilika zoezi la kujaza dodoso la Jamii, siku ya tarehe 22 kuamkia tarehe 23 Mkoa utaendelea na utekelezaji wa zoezi la sensa kuanzia saa sita za usiku kwa kukusanya taarifa za makundi maalum ikiwemo wale wote watakaokuwepo katika madago, Hoteli, mabweni, sehemu za bandarini kwa wale wasafiri wa safari za usiku na uwanja wa ndege, zoezi hili litashirikisha viongozi wa shehia na viongozi wengine.

 

Wito wangu kwa Wananchi

Ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo ni vyema wananchi wakatoa ushirikiano kwa makarani kwa kutoa taarifa zilizo sahihi kwa lengo la kuisaidia serikali katika kupanga mipango ya maendeleo.

Maendeleo haya ni ya wananchi wote na kila mwananchi atakuwa ameshiriki katika kupanga mipango hiyo kwa njia hii, tukumbuke serikali inataka kupanga mipango ya Maendeleo ya Wananchi wake kwa miaka kumi ijayo hivyo ni vyema kutoa ushirikiano kwa makarani ili kupata taarifa sahihi.

Naomba nitoe wito makhsusi kwa wavuvi walioko Dago kurudi Nyumbani si Zaidi ya tarehe 22 kwa ajili ya kuhesabiwa, Viongozi wa dini zote kuhimiza waumini wao, viongozi wa kisiasa kuhamasisha wafuasi wao, Wazee wa Mabaraza na Miji, Vijana, Kinamama, Waalimu wa Madrasa, Mameneja na Wamiliki wa Mahoteli, Wafanyabiashara, Wanamichezo, Madereva na utingo wa Magari ya aina zote, Wakulima, wafugaji na Makundi yote ya Kijamii tujitokeze kwa wingi katika zoezi hili muhimu kwetu na Taifa kwa ujumla.

 

Ndugu Waadhishi wa Habari

Mwisho napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wadau wote na hasa kwenu kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha hamasa na elimu ya ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAAZI ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja.

“Shiriki Sensa kwa kutoa taarifa sahihi, ili upate huduma bora na Manendeleo endelevu”

Ahsanteni

SENSA KWA MAENDELEO TUPO TAYARI KUHESABIWA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.