Habari za Punde

Kuelekea Kombe la Dunia: Tembo Warriors Wajifua Kambini Uturuki Kujiandaa ni Michuano ya Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu, Tembo Warriors leo Septemba 28, 2022 wameendelea na maandalizi yao wakiwa kambi maalum nchini Uturuki waliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na  Michezo kabla ya Oktoba Mosi kuanza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania mjini Pendik.

Mazoezi hayo yameshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt. Hassan Abbasi ambaye amewasili nchini humo Septemba 27, 2022.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa Septemba 30, 2022.


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu, Tembo Warriors wakiwa Nchini Uturiki katika kambi maalum kujiandaa na Michuano ya Kombe la Dunia 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.