MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Msoud
Othman, amesema Dunia imekuwa ikishuhudia mabadiliko makubwa ya kiuchumi ,
Kisiasa na Kijamii na ya Teknlolojia na
kwamba nchi haiwezi kuyaepuka kwa kuwa
ndio yanayoakisi siasa za Ulimwengu na Tanzania kwa jumla.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko hoteli ya Golden Tulip Uwanja
wa Ndege mjini Zanzibar alipofunga mkutano wa Wadau wa Demokrasia uliojadili
masuala makhususi ya Zanzibar yanayohusu
Vyama vingi vya Siasa.
Mhe. Makamu amesema kwamba
siasa za dunia ya sasa ni ushindani , ubunifu na ufanisi na iwapo nchi
itashindwa katika masuala hayo inaweza kuwa ni msindikizaji na hivyo ni vyema
kuicha historia ya kisiasa nchini kuwa mwalimu, lakini sio izuie nchi kusonga
mbele.
Aidha Mhe. Othman amewaeleza
washiriki hao kwamba kuna umuhimu kama taifa kujiuliza sababu za mageuzi
yanayohitajika ndani ya nchi na kukubalika na wananchi na kwamba mtazamo wa kimageuzi lazima ufanane
kifikra kwa wananchi wote ili kuweza
kufikia mageuzi ya kweli ya kidemokrasia.
Amefahamisha kwamba maegeuzi ni muhimu kufanyika katika ustawi wa kiuchumi hasa kwa vile
Zanzibar inategemea sana biashara ya huduma na bidhaa, lakini kwa kutegemea uwekezaji wa fedha
nyingi sambamba na utaalamu wa hali ya juu ili kuvutia uwekezaji utakaoleta
mabadiliko ya kweli ya kiuchumi na
kijamii chini ya kivutio cha amani endelevu nchini.
Aidha amesema kwamba kivutio cha pili kikubwa cha mageuzi ni
sera bora, ni kuwepo taasisi madhubuti na mifumo ya kisasa ya kiserikali ya
kuhudumia biashara na uchumi.
Mhe. Othman ameongeza kwamba kivutio cha tatu ni uwezo wa nchi
katika kushindana na ufanisi wa wengine na kwamba malengo ya mageuzi hayo ni
lazima yawe na maono mapana zaidi wa siasa na ushindani wa kiitikadi.
Amesema kwamba hali hiyo itasaidfia kuhakikisha kuwepo mageuzi
ya kujenga Zanzibar mpya, itakayosimama pahala inapostahiki kwa kuwa mafanikio ya nchi
kama vile Mauritius ambayo ni ndogo kuliko Zanzibar lazima yaifikirishe Zanzibar pahala pa mafanikio hasa kwa vile ina
mazingira bora ya kuweza kufika mbali kimaendeleo.
Mhe. Makamu amesema katika utekelezaji wa kweli wa demokrasia
na ulazima wa mageuzi ya kujenga Zanzibar mpya kuna haja ya kuwa na chombo
makhusi cha kusimamia maridhiano na demokrasia nchini.
Mhe. Amewataka Wazanzibari wote wakiwa ni wazazi na viongozi wanawajibu wa kuwarithisha nchi
iliyotayarishwa kuendana na dunia ya sasa, yenye amani ya kweli, yenye utulivu,
mshikamano na mifumo itakayowapeleka mbele na kwamba Zanzibar hainachaguo
katika hilo.
Mhe. Othman amefafanuya kuwa Ili Zanzibar na Tanzania kwa jumla kutekeleza Dira
hiyo, kunahitajika kuwepo ukweli, katika
kauli na matendo kwa viongozi ili ile dhamira
aliyokusudiwa ya kujenga Zanzibar mpya
iweze kufanikiwa .
Amewataka wazanzibar na watanzania kwa jumla kuelewa kwamba dhamira ya kujenga umoja na Amani ya kweli nchini haipaswi kutikiswa wala kuyumbishwa na changamoto za ndani au nje ya mirengo ya siasa na kiitikadi na kufikiria sana umuhimu wa kuvumiliana.
Mhe. Othman amewataka wanaanchi na Viongozi wa kisiasa
kufahamu kwamba ni lazima kuamini viongozi
wanaweza kujenga misingi ya kuendesha nchi yao kwa misingi inayoakisi
maendeleo ya dunia ya leo.
Hata hivyo, amesema
kwamba katika kujenga demokrsia ya kweli na Zanzibar mpya ni vyema, pamoja na
hadhari ya kutotonesha vidonda, lakini vipatiwe dawa ili vidonda hivyo vibaki kuwa kovu.
Naye waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais , sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza
Hassan Juma,amesema mkutano huo ulikuwa na mafanikio makubwa na kwamba
washiriki walipata fursa ya kujadili kwa uwazi mada mbali mbali
zilizowasilishwa.
Amefahamisha kwamba mada hizo zilikuwa ni chimbuko la mjadala
na washiriki kuelewa vitu vingi na kwamba ni busara wanasiasa kurudi kwa
wananchama kuelezea nia ya dhati ya viongozi wakuu ya kutaka kujenga Zanzibar
na Tanzania mpya katika mustakabali wa maendeleo endelevu.
Amesema kwamba katika masuala ya kujenga Amani, viongozi wa
dini wamekuwa na mchango mkubwa na kuiyomba serikali kuwashirikisha zaidi ili
waweze kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya nchi hasa katika kustawisha
amani.
Amewataka wanasiasa na Viongozi kunga mkono maono na nia
njema ya rais Mwinyi katika kuetekeleza nia ya dhati ya kujenga taswira ya kila
mmoja kushiriki katika maendeleo ya Zanzibar katika kujenga Zanzibar mpya.
Mkutano huo wa Wadau wa Demokrasia kujadili masuala makhusuri ya Zanzibar yanayohusu vyama vingi vya Siasa umeitishwa kufuatia agizo la Rais Mwinyi Kutaka kujadiliwa masuala hayo kutokana na umuhimu wa kipekee kwa Zanzibar
Imetolewa leo na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Kupitia Kitengo cha habari leo tarehe.6/10/2022.
No comments:
Post a Comment