Habari za Punde

Mhe Hemed akutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Na Abdulrahim Khamis , OMPR

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutangaza fursa zilizopo Nchini ili kuwavutia wawekezaji wa kutoka Mataifa mbali mbali.

Mheshimiwa Hemed ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Lawrence Tax alipokutana nae Afisi kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Ameeleza kuwa Wizara hiyo ni muhimu kwa Maslahi ya Taifa na kwani ni kiungo baina ya Watanzania na Mataifa mbali mbali ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempa Wadhifa huo akiamini ana uwezo wa kuisimamia Wizara hiyo.

 Mheshimiwa Hemed amesema  Tanzania unahitajika watendaji watakaosaidia kukuza Uchumi wake kwa kasi kama ambavyo Ilani ya CCM  ya mwaka 2020 - 2025 livyoeleza.

 Aidha Mheshimiwa Hemed amemtaka Waziri huyo kusimamia Mashirikiano ya Kikanda na Kimataifa ili kusaidia kutanua Wigo na kukuza Pato la Taifa.

 Ameeleza kuwa kutambulika kwa Tanzania kutatoa Fursa kwa wawekezaji kutoka Nchi mbali mbali kuja kuwekeza katika sekta mbali mbali  Nchin.

 Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemtaka Waziri huyo kushawishi Mataifa mbali mbali Duniani kuweza kuvutiwa na hali ya Utalii Nchini ili kuweza kukuza Sekta hiyo.

 Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia Waziri huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi itatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanishi na kuweza kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Taifa hili.

 Kwa upande wake Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Lawrence Tax  amemuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa atasimamia uwajibikaji kazini hasa ushirikishwaji wa Zanzibar ndani ya Muungano kwa mujibu wa Katiba.

 Aidha Dkt. Tax  ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano inayoendelea kuipa Wizara anayoiongoza na kumuhakikishia kusimamia ushirikiano huo kipindi chote anachokuwa katika Wadhifa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.