Habari za Punde

Waziri Jenista Mhagama Ashiriki Michuano wa SHIMIWI Mkoani Tanga

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akionesha umahiri wake katika mchezo wa netiboli akiwa akiwa moja ya wachezaji wa timu ya Ofisi ya Rais Ikulu ambao wameifunga kombaini ya viongozi wa SHIMIWI 7-6 ambao umechezwa Oktoba 5, 2022 katika Uwanja wa Bandari jijini Tanga.

Na Mwadishi Wetu, Tanga

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul wameonesha makali yao katika mchezo wa netiboli walipocheza kwenye timu za Ofisi ya Rais Ikulu na timu Muunganiko ya SHIMIWI uliochezwa Oktoba 5, 2022 katika Uwanja wa Bandari jijini Tanga.

Ni dakika 10 tu za mchezo huo zimemtosha Waziri Mhe. Mhagama kufunga magoli 6 kati ya 7 kwa timu yake aliyochezea ya Ofisi ya Rais Ikulu ambayo imeibuka na ushindi wa magoli 7-6 dhidi ya timu Muunganiko ya wanamichezo wa SHIMIWI.

Mchezo huo ni ishara ya kufunguliwa rasmi mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wiraza na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) 2022 yanayoendelea jijini Tanga ambayo yalianza kurindima rasmi Oktoba 1-15, 2022.

Mashindano ya mwaka huu ni ya 36 tangu kuanzishwa kwake na yakishirikisha wanamichezo 2,510 kutoka Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala na Mikoa yakiongozwa na kaulimbiu “Michezo hupunguza magonjwa yasiyoambukiza na huongeza tija mahala pa kazi”.

Aidha, mchezo ya ufunguzi rasmi wa mashindano ya ya SHIMIWI, mpira wa miguu ulizikutanisha timu za Wizara ya Kilimo na Bohari ya Dawa (MSD) ambapo Kilimo wameibuka kidedea kwa jumla ya magoli 3-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakani jijini humo.

Kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Mahakama wameichabanga timu ya Wizara ya Kilimo kwa jumla ya magoli 28-26 chezo ambao umechezwa katika uwanja wa Bandari jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.