Habari za Punde

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi unaendelea Sharm El-Sheikh, Misr

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akisalimiana na Bi. Janet Rogan mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Katika kikao hicho Tanzania na Uingereza zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili.

Mjumbe kutoka Serikali ya Uingereza Bi. Janet Rogan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na ujumbe wake katika kikao cha ushirikiano kilichofanyika katika Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri leo tarehe 16 Novemba 2022. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland katika banda la Tanzania kwenye Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Sharm El-Sheikh, Misri. Bi. Scotland ameipongeza Tanzania kwa jitihada za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.