Habari za Punde

MNEC Mtewela Awataka Wanachama wa CCM Kuwa na Umoja

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akitoa cheti cha pongezi kwa wanaccm mwandamizi
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akitoa nasaa kwa wanachama wa chama cha mapinduzi juu ya kudumisha umoja wa chama hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akitoa cheti cha pongezi kwa wanaccm Leah mwamoto

Na Fredy Mgunda, Iringa.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kufanya kazi kwa ushikamana katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi ili kuimarisha ustawi wa Chama na kuunga mkono maono ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama hicho Taifa katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Akitoa Salam za Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan,Mtewele amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa kumi wa Uchaguzi wa CCM mkoa wa iringa ambapo amesema ili kuwa na maendeleo thabiti kuwa na viongozi imara ndiyo nguzo katika kufikia ndoto za wananchi anaowaongoza huku akisisitiza suala la umoja na mshikamano baina yao.

Mtewele alisema kuwa chama cha mapinduzi kinajengwa kuanzia kwenye matawi,shina,kata, wilaya hadi Taifa hivyo wanachama wote wanatakiwa kuwa na ushirikiano ili kukiwezesha chama kuwa imara na kuongeza wanachama wapya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.