Habari za Punde

Watendaji Wizara ya ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wahimizwa kufanya kazi kwa bidii

 


Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji bi Mariam Juma Abdullah amewataka watendaji  wa Wizara ya Maendeleo  ya Jamii jinsia  Wazee na Watoto kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na mashirikiano ili kuiletea Maendeleo Wizara yao.

Katibu bi Maryam ameyasema hayo Leo wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdalla yaliyofanyika Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Bi Maryam amesema mashirikiano ni jambo la msingi katika kuleta mafanikio mazuri katika kazi.

Aidha amewataka watendaji hao pia kumpa ushirikiano wa kutosha Katibu Mkuu wao Mpya kama walivyompa yeye ili nae aweze kuiendesha vyema Wizara hiyo.

Pia  amewasisitiza watendaji wa hao kuhakikisha  wanaendeleza nidhamu  na kufuata utaratibu uliowekwa wa katika utendaji wa kazi na kuwasisitiza kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwani inaweza kuharibu mustakbali mzima katika majukumu yao.

Hata hivyo Bi Maryam ametumia muda huo kuwashukuru wafanyakazi wote wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katakana na ushirikiano mzuri waliompa katika kipindi chote alichokuwa akiiongoza Wizara hiyo pamoja na kuwaomba msamaha pale alipokosea na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kadiri atakapohitajika katika Wizara hiyo.

Nae  Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Maendeleo  ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto bi Abeida  Rashid Abdallah amemshukuru Katibu Bi Maryam kwa ushirikiano aliokuwa akimpa pamoja na maelekezo na kumuonba kuendelea kumpa mashirikiano hayo ili aweze kutekeleza vyema majukhmu yake.

Hata hivyo amemshukuru kwa kukabidhiwa vyenzo na  vifaa vya kufanyia kazi ambapo amewaomba watendaji  wa Wizara hiyo kushirikiana ili malengo ya Wizara hiyo yaweze kufikiwa kama yalivyokusudiwa.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO ZANZIBAR 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.