Habari za Punde

Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja Watakiwa Kufanya Majukumu ya Kazi Zao

Mbunge wa viti Maalum wanawake Mkoa wa Kusini Unguja Mwatum Dau Haji  akizungumza na wajumbe (hawapopichani) waliofika katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la Wilaya ya Kusini Unguja na kujadili ripoti ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi wa (CCM) mwaka 2020 hadi mwaka 2025 uliyofanyika katika tawi la Makunduchi Mkoa huo.
Mbunge wa viti Maalum wanawake Mkoa wa Kusini Unguja MwatumuDau Haji  akipatiwa neno la shukurani na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Kusini Mwanamvua Mwinyi Juma mara baada ya kuzungumza na wajumbe walifika katika ufunguzi wa Mkutano wa baraza la Wilaya ya Kusini Unguja uliyofanyika katika tawi la Makunduchi Mkoa huo.

Na Miza Othman Maelezo Zanzibar.

Jumuya ya umoja wa Wazazi Mkoa wa Kusini Unguja wametakiwa kufanya majukumu ya kazi zao ili kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya Mkoa huo.

Haya yalielezwa na Mbunge wa Vitu Maalumu Mkoa wa Kusini Unguja Bi Mwatum Day Haji wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wilaya Mkoa wa Kusini Unguja  katika tawi la Makunduchi ndani ya Mkoa huo.

Alisema lengo la ufunguzi wa Mkutano huo ni kuwataka wanajumuiya hao kusimamia Chama hicho kwani kufanya hivyo kutapelekea kutoyumba kwa uchaguzi ifikapo mwaka 2025. 

Hata hivyo amewataka wanajumuiya hao kuwa na umoja, Ushirikiano na Upendo wakati wanapotekeleza majukumu yao kwalengo la kukiletea maendeleo Chama Chao.

Kwa upande wao wanajumuiya hao wamesema watayafanyia kazi na kuyatekeleza yaleyoye aliyoahidi kwani kufanya hivyo ni kuisaidi na kuipa msukumo Serikali iliyopo madarakani kwa sasa.

Nao wajumbe hao  wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuitikia wito wao na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ndani ya jumuiya yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.