Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amwakilisha Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Nchini Angola

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na  Rais wa Angola Joao Lourenco, alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Interconinental kuhudhuria Mkutano  wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika, Angola jijini Luanda, Disemba 9, 2022. Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, walipokutana katika Ukumbi wa Kimataifa wa Interconinental mapema kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika Angola jijini Luanda, Disemba 9, 2022.Waziri Mkuu anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano huo. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na viongozi wengine kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia hoja zinazotolewa katika Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika nchini Angola
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiaya ya Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) unaofanyika nchini Angola Disemba 9, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.