MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amefanya ziara maalum ya
kuwatembelea na kuwajulia hali wagonjwa mbali mbali katika maeneo tofauti ya
Mkoa wa mjini Magharib Unguja.
Akiwatembelea
wagonjwa hao majumbani kwao, Mhe. Othman amewataka wagonjwa wote
kuendelea na uvumilivu na subra kutokana na maradhi waliyonayo na
kumuomba Mwenyezi mungu awape shifaa ili
wapone haraka na waendelee na shughuli
zao binafsi na kushiriki katika kazi ujenzi wa taifa.
Mhe.
Othman, amewaeleza wagonjwa aliowatembelea kwamba maradhi ni mtihani kutoka kwa
mola Muumba kuwakumbuka waja wake kwa namna tofauti na ni yeye pia mwenye uwezo
wa kuponya maradhi yote.
Mhe. Othman
katika ziara hiyo alimtembelea Kadhi Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji huko nyumbani kwake Magogoni na
Mwengine aliyemtembelea nyumbani kwake Magomeni kwa Ayuba ni Sheikh Khamis
Yussuf ambaye ni Amiri wa Jumuiya ya Answari Sunna na pia ni Naibu Katibu wa Jumuiya
ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA).
Aidha
alimtembelea Katibu Mtendahi wa Jamuiya ya Maimamu Zanzibar huko nyumbani Kwake
eneo la Saraevo katika wilaya ya Magharib B Unguna Sheikh Muhidin Zubeir na pia
alimujulia hali ndugu Ali Abdalla Ali huko nyumbani kwake Chukwani Zanzibar.
Nao
wagonjwa waliotembelewa wealimshukuru Mhe. Othman kwa uamuzi wa kuwajulia hali
na kusema kwamba wamefarajika sana na
ujio wa mhe. Makamu majumbani kwao ili
kuwajulia hali na kumuomba aendelee na utaratibu huo kwa kuwa ni jambo jema na
linaridhiwa mwenyezi mungu Muumba.
Mhe.
Othman amekuwa akiwajulia hali wagonjwa na watu mbali mbali
wasiojiweze katika kila baada ya vipindi
ikiwa ni utaratibu wake aliojiwekea.
Ziara kama hiyo aliifanya katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo aliwatembelea wazee na wagonjwa mbali mbali katika wilaya za Mjini na Magharib Unguja.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Kupitia Kitengo chake cha
Habari leo tarehe 24.01.2023.
No comments:
Post a Comment