Habari za Punde

Mhe Othman ashiriki maziko ya Marehemu Samir Hafidh Hassanali (Samir Rose)


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Januari 30, 2023 amejumuika na wananchi na viongozi mbali mbali wa Serikali, Dini na Siasa katika maziko ya Marehemu Samir Hafidh Hassanali maarufu kwa jina la 'Samir Rose'

Ibada ya Sala ya Maiti na Dua ya kumuombea Marehemu imeongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaab, hapo katika Msikiti wa Miembeni, Mkoa wa Mjini- Magharibi, Unguja.

Al Marhum Samir aliyekuwa mfanyabiashara ndogo ndogo maarufu katika mtaa wa Mtendeni, amefariki dunia jana Januari 29 huko Fuoni na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.