Bahati Habibu
Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Salum Ameir Issa amewata vijana Nchini kuitumia michezo kuwa fursa ya kujiajiri na njia itakayowafanya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji pamoja na kujiepusha na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo ameitowa huko shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi “B” mkoa wa Mjini Magharibi wakati akifungua Bonanza la Michezo la kuwahamasisha Vijana wa Shehia hiyo kujiunga na Baraza hilo.
Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la kesi zinazo wakabili vijana kwa makossa yatokanayo na vitendo vya udhalilishaji na matumizi ya dawa za kulevya jambo ambalo ni hatari hasa ikizingatiwa vijana ndio tegemeo la dadae kwa ujenzi wa Taifa.
Amesema hali hiyo ilisababishwa na vijana kujiachia na kuzurura bure na hatimae kutumbukia katika hali mbaya ya vitendo vibovu.
Amesema vijana wajiunge na baraza hilo ili liweze kuwasaidia na kuweza kuwatatulia changamoto zinazo wakabili.
“Nakuombebi vijana mjiunge na baraza hili ili kupata fursa zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia taasisi hiyo”alisema katibu Salum Ameir.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza la Vijana inaendelea kuwapatia vijana elimu ya ujasiriamali kwa kuwapeleka Vijana katika Vyuo vya Mafuzo vya amali sambamba na kuwapatia mitaji itakayo wafanya wajiajiri baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
“Niwaambie Vijana wenzangu ni muhimu kujiunga na Baraza hii itatusaidia kuwa na uzalendo wa kulinda nchi yetu na kutambua fursa za kiuchumi zilizomo nchini.” Alisema Katibu huyo.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Pangawe Iddi Ali Ame amesema michezo imekuwa ni sehemu ya ajira hivyo amewataka vijana kushiriki michezo kwa lengo la kuimarisha afya na kuonyesha vipaji vyao vitakavyowasaidia kujiajiri au kuajiriwa.
Katika bonaza hilo Michezo mbali mbali imechezwa ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu na mpira wa nage sambamba na utolewaji wa fomu za kujiunga na Baraza la Vijana Zanzibar kwa washiriki wa Bonanza hilo.
No comments:
Post a Comment