Habari za Punde

Malezi kwa Watoto Yanahitajika ili Kuwasaidia kukua Katika Makuzi Bora

Na.Maulid Yussuf. ZANZIBAR

Mashirikiano ya malezi kwa watoto yanahitajika ili kwasaidia watoto kukua katika makuzi bora pamoja na kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji nchini. 

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Siti Abbas Ali ameyasema hayo katika muendelezo wa utoaji wa elimu juu ya masuala ya udhalilishaji katika shehia mbalimbali nchini.

Akizungumza katika shehia ya Mnarani Kijitoupele, Mkurugenzi Siti amesema bado wazazi wanaume wamekuwa wakiwaachia ulezi kina mama pekee hali ambayo inapotokea tatizo lawama pia zinawakuta wao.

Aidha amewataka wazazi kupunguza kuwakaripia ovyo watoto na badala yake kuwaweka karibu ili wanapofikwa na tatizo waweze kusema na kuweza ufuatilia.

Pia amewataka kupunguza hasira kwa kutowapa adhabu kubwa watoto wanapofanya makosa kwani baadhi yao wamekuwa wakiwachoma moto watoto jambo ambalo linaweza kumsababishia ulemavu wa maisha Mtoto huyo.

Hata hivyo amewanasihi wanaume kuwaunga mkono wanawake katika shughuli zao mbalimbali za kimaendeleo na hata wanapohitaji kugombea nafasi za uongozi ili kuleta mafanikio zaidi katika jamii.

Nae Sheha wa shehia ya Mnarani bwana Ramadhan Abdallah Rajab amewataka wananchi wa shehia hiyo kuwa karibu na ofisi zao za shehia kwani matukio mengi yanayofanyika yanatokea katika shehia, huku akiahidi kuendelea kutoa huduma bora katika shehia yake.

Kwa upande wao baadhi ya  wakaazi wa Shehia ya Mnarani wamewanasihi wazazi wenzao kutowapa simu watoto wao kwani ni miongoni mwa vichocheo vya kuwepo matendo ya udhalilishaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.