Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Amtembelea na Kumjulia Hali Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar Bw. Mohammed Raza Aliyewahi Kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla  amefika kumjulia hali aliekuwa Mwakilishi  wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammed Raza Hassanali, huko Nyumbani kwake Ali Abbas Tower Mtaa wa Jamhuri  Jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Mhe. Hemed ameongozana na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbali mbali.

Mhe. Hemed amemueleza Mhe. Raza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi zake anazoendelea kuzichukua hasa maamuzi yake ya kusaidia ujenzi wa Vyoo Kumi na mbili vya wanafunzi wa Kike Skuli ya Madungu Kisiwani Pemba pamoja na ahadi yake ya kuendelea kuinua vipaji na kuendeleza michezo Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kufurahishwa kwake kuona hali ya Kiongozi huyo inazidi kuimarika siku hadi siku na kumfikishia   salamu za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo anamuombea kwa M/Mungu Mtukufu apone haraka ili kuendelea na majukumu ya kuijenga Zanzibar.

Nae aliekuwa Muwakilishi wa Jimbo la  Uzini Zanzibar Mhe. Muhamed Raza Hassanali amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na ujumbe aliofuatana nao kwa kufika  kumjulia hali hatua ambayo inaonesha wazi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea inathamini jitihada zake katika kuiletea maendeleo Zanzibar.

Aidha Mhe. Raza amemuomba Mhe. Hemed kumfikishia salamu zake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kuwatumikia wazanzibari kwa miradi mbali mbali ya maendeleo na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiambatana na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walifika Hospitali ya Saifee Mtaa wa Osterbay Dar - es - Salaam kumjuulia hali Muwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (ACT Wazalendo) Mhe. Habib Ali Muhamed anaeendelea kupatiwa Matibabu Hospitalini hapo.

Mhe. Hemed amewataka wanafamilia kuwa wamoja hasa katika kipindi hichi wanachomuuguza Mzee wao pamoja na kumuombea Dua ili apone haraka aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia Wananchi wa Jimbo la Mtambwe.

………………….

Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.