Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya Picha ya Jengo la Kihistoria la Zanzibar, Bait el Ajaib, Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na  Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum ambae ni Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.