Habari za Punde

Utiaji wa Saini Mkataba wa Ujenzi wa Beit - Al Ajab Zanzibar

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mheshimiwa Simai Mohamed Said ameshiriki katika kusaini Mkataba wa ujenzi wa Jengo la Beit al ajab huko Maskati Oman ambapo Jengo hilo litagharibu dola Milioni 21 ambazo ni zaidi ya Bilioni 55 za Tanzania.

Mheshimiwa Simai amesema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kuanza mapema ndani ya miezi mitatu baada ya utiaji saini wa mkataba huo, fedha hizo zitatumika katika kutayarisha mambo yanayohitajika kufanikisha ujenzi huo.

Jengo hilo la kihistoria linatarajia kuwa na Makumbusho kubwa ya kisasa kwa ajili ya kuihifadhi na kuitangaza historia ya Zanzibar kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Aidha, Mhe.Simai amesema, utiaji saini wa Mkataba huo kutapelekea kuzileta Nchi hizo karibu pamoja na kukuza na kuendeleza ushirikiano uliyopo na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale itaendelea kushirikiana na Serikali ya Oman katika kuliendeleza na kulisimamia Jengo hilo ambalo ni urithi Mkubwa na mashuhuri Barani Afrika.

@officialomantravels @omanis_vip @simai_msaid @fatma.m.khamis
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman Mhe. Ibrahim Al Harous, wakati wakibadilisha mawazo baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya ujezni wa jengo la Beit Al-Jaib utakaogharimu dola za kimarekani milioni 21, hafla hiyo iliyofanyika Nchini Oman.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman Mhe. Ibrahim Al Harous, wakati wakibadilisha mawazo baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya ujezni wa jengo la Beit Al-Jaib utakaogharimu dola za kimarekani milioni 21, hafla hiyo iliyofanyika Nchini Oman.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.