Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Amefungua Kikao cha Kamati ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania

Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensaya Watu  na Makazi, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Hemed Suleiman Abdulla wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kikataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam kushiriki katika Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi.


Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya  Sensa ya Watu  na Makazi , Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 25-2-2023.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza Kikao cha Tisa cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar-es-salaam.

Akifungua Kikao hicho Mhe. Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 ameeleza kuwa kukamilika kwa zoezi la Sensa mwaka jana limetokana na kamati hiyo kusimamia miongozo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo walifatilia kwa ukaribu muendelezo wa zoezi hilo kwa kila  hatua.

Sambamba na hayo Mhe. Majaliwa ameishukuru Kamati hiyo kwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kuandaa na kusimamia zoezi hilo hadi kukamilika kwake.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Uratibu na Bunge Mhe. George Simbachawene ameeleza kuwa matokeo ya awali ya Sensa ya watu na makazi ya mwezi Agosti 2022 yamechanganua takwimu kuanzia ngazi ya Kata kwa Tanzania Bara na Shehia kwa Tanzania Zanzibar.

Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Anwani za Majengo Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali ameeleza kuwa Zoezi hilo ni la mara ya kwanza kufanyika Tanzania ambalo linasaidia kukamilisha mipango kazi ya maendeleo ikiwemo utungaji wa Sera.

Akiakhirisha Kikao hicho Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewashukuru wajumbe wa kikao hicho kwa kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Aidha, Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa takwimu za zoezi hilo zinaakisi mahitaji ya watanzania na amewataka watendaji wote Serikalini kuwa kuhakikisha  takwimu hizo zinaendana na mipango ya sahihi ya Serikali ili watanzania wanufaike.

Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya sensa ya watu na makazi kimejumuisha Mawaziri na Makatibu Wakuu, Watakwimu wakuu, na makamisaa wa sensa ya mwaka 2022, na watendaji wa taasisi na sekta mbali mbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.