Habari za Punde

Kongamano la Idhaa za Kiswahili Kufanyika Kesho Zanzibar Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar

Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokua akitoa taarifa kuhusiana na kongamano la idhaa ya Kiswahili lenye lengo la kutathmini matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari Duniani,  linalotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 katika Ukumbi wa Sheikhe Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni . hafla iliyofanyika Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar. machi 17,2023.
Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokua akitoa taarifa kuhusiana na kongamano la idhaa ya Kiswahili lenye lengo la kutathmini matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari Duniani,  linalotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19 katika Ukumbi wa Sheikhe Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni . hafla iliyofanyika Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar. 
Katibu mtendaji  Baraza la Kisawhili Zanzibar BAKIZA Dkt.Mwanahija Ali Juma  akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali  wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu kongamano la idhaa ya Kiswahili  linalotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19  katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni Mjini Zanzibar  , hafla iliyofanyika Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatib akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali  wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliohusu kongamano la idhaa ya Kiswahili  linalotarajiwa kufanyika tarehe 18 na 19  katika Ukumbi wa Sheikhe Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni , lililoandaliwa na Baraza la Kisawhili Zanzibar BAKIZA, kwa kukishirikiana na Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA na Idara ya Utamaduni na kushirikisha wadau mbalimbani wa Habari  ndani na nje ya Tanzania, likiwa na kauli mbiu “KISWAHILI NI NYENZO YA MAWASILIANO TUJIAMINI KUKITUMIA “hafla iliyofanyika Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar. machi 17,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
 

Na Khairat Mohd        Maelezo    17/3/2023

Baraza la Kiswahili Zanzibar wakishirikiana na Baraza la Tanzania pamoja  na Idara ya Utamaduni Zanzibar wanatarajia kufanya kongamano  la idhaa la Kiswahili duniani ili kuwakutanisha wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Tabia Maulid Mwita akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Migombani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Aidha amesema kongamano hilo litajadili fursa na changamoto za mawasiliano ya habari katika maendeleo ya matumizi ya lugha ya  Kiswahili.

Waziri Tabia amesema katika kongamano hilo kutahusishwa mambo mbalimbali ikiwemo uwasilishaji wa Makala,mijadala na tunzo ya umahiri wa waandishi wa Kiswahili na kushajihisha matumizi fasaha ya usanifu wa lugha hiyo katika vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa.

Vilevile kutakuwepo na ziara  ya kitalii katika vituo vya Radio, Televisheni na kaburi la Hayati Abeid Amani Karume huko kisiwandui pamoja na kutembelea kisiwa cha Prison Island.

Aidha katika shunguli hiyo kutakuwa na tunzo za umahiri wa andishi wa Kiswahili na kushajihisha matumizi fasaha ya usanifu wa kiswahil  vyombo ambavyo vitashiriki katika tunzo hizo ni Televisheni,radio Gazeti na mitandao ya kijamii pamoja na waandishi wanaotumia Kiswahili sanifu katika vyombo hivyo.

Pia ufungaji wake utafanyika tarehe 19 ukumbi  wa Sheikh Idrisa Abdul wakil unaotarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa Majaliwa.

Hivyo anawataka Wandishi wote kushiriki kwenye kongamano hilo kwani litawajengea uwezo  katika matumizi ya lugha ya Kiswahili .

Kongamano hilo la siku mbili linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Kiswahili kutoka ndani na nNje ya Tanzania ambapo kauli mbiu  inasema Kiswahili ni nyenzo ya mawasiliano tujiamini kukitumia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.