Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Azungumza Katika Maadhimisho ya Malaria Duniani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Baraza la Taifa la Kupambana na Maambukizi ya Malaria baada ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duaniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Aprili 25, 2023. Kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Leodgar Tenga. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza la Taifa la Kupambana na Maambukizi ya Malaria baada ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duaniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Aprili 25, 2023. Kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, mratibu wa masoko wa kampuni  ya kutengeneza dawa ya kuangamiza mbu iitwayo  Tanzania Biotech Products Limited, Pilly Abbas   (kulia) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Aprili 25, 2023.  Wa pili kulia ni  Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Mhandisi  Raphael  Rodriguez.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi  pamoja  na wajumbe wa Baraza la Taifa la  Kupambana na Maambukizi ya Malaria baada ya kuzindua Baraza hilo katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Aprili 25, 2023.  Kulia kwake ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Leodgar Tenga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.