Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Awasilisha Hutuba ya Bajeti ya Ofisi Yake leo

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwasilisha Hutuba ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Mkutano wa 11 wa Baraza la 10 la Wawakilishi, ulioaza leo katika ukumbi wa Baraza Chukwani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.  
 

Na.Abdulrahim Khamis. OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha wananchi wote walioathirika na utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia wanalipwa fidia zao kikamilifu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya mapato  na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Kikao cha kwanza cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Ameeleza kuwa Serikali tayari imeshalipa jumla ya shilingi Milioni 947 kwa wananchi walaioathirika na utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia ambapo kiasi cha fedha kilichobakia kitalipwa kwa wananchi hivi karibuni.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga kuanza ujenzi wa bohari ya kuhifadhia mafuta yenye uwezo wa mita za ujazo milioni thalathini (30,000,000) jambo ambalo itasaidia Zanzibar kuagiza mafuta hatua ambayo itapunguza gharama za mafuta nchini.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed Amesema Uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika ambapo kasi ya ukuaji wa umefikia asilimia 6.8 kwa mwaka 2022 ikilinganishwa na ukuaji wa wastani wa asilimia 5.1 mwaka 2021 iliyochangiwanna kuimarika kwa sekta ya viwanda, uingiaji wa watalii nchini kuongezeka kwa usafirihaji wa mazao ya biashara pamoja na  kuongezeka uwekezaji.

Akigusi Pato la Taifa Mhe. Hemed ameeleza kuwa mwaka 2022 Pato la Taifa limeongezeka kutoka Shilingi Trilioni 3.275 mwaka 2021 na kufikia thamani ya shilingi Trilioni 3.498 huku kasi ya  mfumko wa bei kwa mwaka 2022 imeongezeka na kufikia wastani wa asilimia 5.1 kutoka wastani wa asilimia 1.7  mwaka 2022 ambapo ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa bei bidhaa zote cha za chakula na zisizo za chakula.

Aidha ameeleza kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara za mijini na vijijini, ujenzi wa Uwanja wa Ndege Pemba, ujenzi wa Bandari ya Mangapwani pamoja na kuimarisha miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo Afya, Elimu, Maji safi na salama na ujenzi w viwanja vya michezo kwa kila Wilaya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kwa hatua wanazoendelea kuzichukua katika kuhakikisha kuwa shughuli za kisiasa zinaendeshwa kistaarabu.

Aidha amewataka Viongozi wa kisiasa na wananchi kuendelea kuheshimiana katika mitazamo kwa kuzingatia uzalendo kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kutekeleza vyema maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 na kupongeza hatua ya wananchi kupewa taarifa za utekelezaji wa Ilani hiyo kutoka mamlaka husika kwa nyakati zilizopangwa.

Katika Hotuba hiyo Jumla ya shilingi 75,316,075,026 zimeombwa kuidhinishwa kwa matumizi ya Oisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

10/05/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.