Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi leo tarehe 31 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Nayishimiye mara baada ya kuwasili Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi kushiriki Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo tarehe 31 Mei 2023.
No comments:
Post a Comment