Habari za Punde

Ubalozi wa Norway Tanzania wataka wanawake wengi zaidi kuwa viongozi Zanzibar

Na.Mwandishi Wetu  

Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuwaunga mkono wanawake Zanzibar ili kushika nafasi za uongozi.

Aliyasema hayo leo tarehe Mei12, wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa haki za wanawake katika ukumbiwa TAMWA Tunguu Zanzibar.

Aidha alisema Norway imekuwa ikishirikiana na Tazania kwa miaka 60  sasa katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo masuala ya kuwaunga mkono wanawake katika uongozi.

Alisema pia wataendelea kufungua milango zaidi kukaribisha asazi za kiraia, waandishi wa habari na jamii wakiamini kuwa wana mchango mkubwa kwenye jamii na hivyo wanapaswa kuungwa mkono.

Akifafanua zaidi alisema anaamini kuwa suala la wanawake kuwa viongozi linaweza kuchukua muda mrefu, lakini kama watajengewa uwezo watakuwa na udhubutu na kujiamini ya kushughulikia changamoto kuanzia ngazi ya familia.

Katika hatua nyengine, Balozi huyo alieleza kusikitishwa kwake na vitendo ya udhalilishaji kwa wanawake na kusema kuna haja ya kuunganisha nguvu zaidi katika mapambano hayo huku lengo likiwa ni kuwaweka wanamke katika mazingira salama.

Awali Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema wamekua wakifanyakazi ya kuwajengea uwezo wanawake mbali mbali Zanzibar na kwa kiasi fulani kuna mafanikio makubwa na wapo ambao wameshakua viongozi.

Akichangia kati mkutano huo Bi Asha Aboud alisema kuna umuhimu kuendelezwa kwa ukaribu zaidi unaofanywa na watekelezaji wa mradi huu ili kuendelea kuwafikia walio wengi zaidi.

Nae Mkurugenzi wa Jumuia ya wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud alisema wameweka mikakati imara hatua nyengine ya utekelezaji mradi huo ikiwemo kuwajengea uwezo zaidi wahamishaji jamii.

Ziara ya Balozi wa Norway Tanzania imekuja kufuatia utekelezaji mrari wa kuhamaisha wanawake wa Zanzibar kushiriki kwenye nafasi za uongozi (SWIL) ambao unatekelezwa na TAMWA-ZNZ,ZAFELA pamoja na PEGAO kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.