MUONEKANO
wa Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja uliofunguliwa leo 12-5-2023 na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali
Mwinyi, na kujumuika na Wananchi wa Paje katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika
katika msikiti huo baada ya ufubguzi wake
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiondoa pazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Msikiti Mkuu
wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja (kushoto) Mfadhili wa ujenzi wa Msikiti huu Dkt.
Mahir Bakar,hafla hiyo ya ufunguzi wa msikiti huo uliyofanyika leo 12-5-2023 na
kujumuika na Wananchi wa Paje katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, baada ya ufunguzi
wake
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akikata utepe kuufungua Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja leo
12-5-2023, na (kulia kwa Rais) Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti huo Dkt. Mahir
Bakar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora
Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja baada ya
kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo baada ya
kufunguliwa leo 12-5-2023
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akijumuika na Wananchi wa Paje kuitikia dua ikisomwa na Katibu Mtendaji wa
Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, baada ya kumalizika
kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya
Kusini Unguja na (kushoto kwa Rais) Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti huo Dkt. Mahir
Bakar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria,Utumishi
na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi
akiwasalimia Watoto wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kumalizika kwa
Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Paje leo 12-5-2023,
baada ya kuufungu na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadid
Rashid Hadid.
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amechangia shilingi
milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa maduka matano, yanayokusudiwa kutoa gharama za
uendeshaji wa msikiti mkuu wa Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.Al hajj Dk. Mwinyi alitoa mchango huo alipofungua msikiti
huo na kuiasa jamii na waumini msikitini hapo, kujitoa kwa hali na mali kuchangia
ujenzi wa maduka hayo ili kukamilisha ujenzi.
Alisema ujenzi wa maduka hayo utachangia gharama za
uendeshaji wa misikiti huko endapo utahitaji matengenezo na ukarabati, gharama
za maji na umeme pamoja na gharama za kuwalipa masheikh na maimamu
watakaouendesha msikiti huo.
Aidha, Al hajj Dk. Mwinyi aliwanasihi waumini na viongozi
wa msikiti huo kuutumia vyema kwa mambo ya khairati na yenye kujenga jamii
iliyobora, ikiwemo kusaliwa, kuwafundishia vijana maadili mema na kuwakataza
mabaya, ili kuwanusuru na majanga ya kilimwengu ikiwemo athari za dawa za
kilevya na masula ya udhalilishaji wa kijinsia.
Pia, aliwaeleza waumini hao lengo la kujengwa
misikiti hiyo kwa waumini ni kusaliwa kwa wakati na kufanyiwa ibada kwa wingi,
hivyo aliwaomba kujaza safu wakati wote wa kutekelezwa kwa ibada msikitini
hapo.
Al hajj Rais Dk. Mwinyi, pia alitumia fursa hiyo
kuwashukuru wafadhili wa ujenzi wa msikiti huo pamoja na kuwashukuru wazawa kwa
weledi wa kujitoa kwao kuanza ujenzi wa msikiti huo kabla ya kupata wafadhili.
“Tunawashukuru sana wafadhili wetu kwa kujitoa na
kuijenga misikiti mizuri na yenye hadhi kubwa kama huu, lakini ningependa zaidi
niwashukuru, niwapongeze na niwatakie kila la kheir wale ndugu zetu walioanza
ujenzi wa msikiti huu kabla ya kupata wafadhili, hawakukaa wakafunga mikono
wakasema tunamsubiri mfadhili, walianza wao. Hii ni imani kubwa walioionesha
kidogo walichokua nacho walianza nacho hadi walimaliza msingi wa jengo lote.”
Alipongeza Al hajj Dk. Mwinyi.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisema,
wananchi na waumini wa Mkoa wa Kusini Unguja wanaungamkono jitihada
zinazofanywa na Rais Al hajj Dk. Mwinyi.
Akizungumza kwenye halfa ya ufunguzi wa msikiti huo,
Mfadhili Dk. Maheer Bakari alieleza misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu, hivyo
aliwaomba waumini wazitukuze, wazitunze na kuziheshimu kwaajlili ya kimtaja
Mwenyezi Mungu muda nyakati zote.
Pia alimshukuru Rais Al Hajj Dk. Mwinyi kwa harakati
zake kwenye masuala ya dini.
Pia sheha wa Paje, Mohamed Rajab nae alieleza ujenzi
wa msikiti huo ulianza mwaka 2021 kwa wananchi wa shehia hiyo kujitolea
kuchimba msingi na kuutengeneza wote na mwaka jana walitokea wafadhali na
kuujenga msikiti huo hadi kukamilika kwake.
Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafadhili hao kwa
kuukamilisha ujenzi wa msikiti huo.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment